Vitu vitano (5) vya muhimu kuweka kwenye chakula cha kuku | KUKUKIBIASHARA
Breaking News
Loading...

Ad

Jumapili, 10 Desemba 2017

Vitu vitano (5) vya muhimu kuweka kwenye chakula cha kuku

Habari ndugu msomaji na mfuatiliaji wa blog hii, karibu tena tuweze kuelimishana kwa kupata maarifa zaidi na jinsi ya kupambana na changamoto za ufugaji kiujumla ili tuweze kutumia fursa hii ya Tanzania ya viwanda na kuweza kuhudumia kitoweo badala kuwaachia wachache waagize nje ya nchi, wakati wazawa tunazalisha pia.
Niingie moja kwa moja kwenye mada yetu ya leo kuhusu vitu muhimu vinavyotakiwa kwenye chakula cha kuku.Kuna vitu vitano muhimu vinavyotaijika kwa kuku ili awe na afya bora. Navyo ni kama vifuatavyo.

1. Protini.
2. Mafuta.
3. Wanga.
4. Madini.
5. Vitamini.

1.PROTINI
Ni aina ya vyakula ambavyo kazi yake kubwa ni kukuza mwili navyo ni kama ifuatavyo,
-Mtama, Dagaa, Alizeti na Soya
Hivi vyote inategemeana na maeneo uliko, nini kinapatikana kwa urahisi.

2. WANGA.
Ni aina ya vyakula ambavyo kazi yake ni kuupa mwili nguvu. Navyo ni kama ifuatavyo
-mahindi yaliyo balazwa
-pumba ya mahindi
-pumba ya mpunga

3. MAFUTA.
Ni aina ya vyakula ambavyo kazi yake kubwa ni kuupa mwili joto pamoja na kulainisha mmeng'enyo wa chakula mwilini. Kundi hili kuna vitu vifuatavyo
- mashudu ya alizeti
- mashudu ya pamba

4. MADINI
Hapa kuna madini ya aina mbalimbali ambayo kazi yake kubwa ni kuimarisha mifupa na ganda la juu la yai pia. Na haya madini ni muhimu sana, kwa sababu yanakazi kubwa katika mwili wa kuku. Yanamwezesha kuku kutembea vizuri na kwa ukakamavu. Pia yai la kuku ili liwe imara lenye ganda gumu lazima apate madini ya kutosha. Bila kusahau madini yanasaidia kuku kutonyonyoka manyoya yake. Madini hayo ni kama ifuatavyo,
- Mifupa
- Chokaa ya kuku
- D.C.P - Dicalcium Phosphate. ( hizuia kudonoana, kula mayai, maganda malaini. Pia huimarisha maganda ya mayai, husaidia kuongeza mayai )

5. VITAMINI.
Ni aina ya vyakula ambavyo vinapatikana sana kwenye mbogmboga n.k lakini kazi yake kubwa ni kuimarisha mwili uwe vizuri kama vile kuona, kuwa na manyoya imara na afya bora. Kundi hili linavyakula kama vifuatavyo
- mchicha
- chainizi
- spinachi
- majani ya paipai

KUMBUKA:
Pia katika maduka ya mifugo kuna vitamini zinauzwa ambazo hutumika pia kama mbadala wa mazingira yetu yalivyo kuna baadhi ya maeneo kupata mbogamboga ni changamoto. Kuna "vitalyte" ni nzuri kwa kuku na hata nyingine pia.

Pia kuna kitu kingine vya msingi katika chakula cha kuku.

PREMIX
Ni aina ya virutubisho amabvyo hutumika kulingana na aina ya kuku. Inaleta matokeo chanya kwa kuku Muda mwingine huitwa busta. Nazo zipo katika mahindi mawili ambazo ni..
1. Layers concentrate
2. Broiler concentrate

MAJI.
Maji ni kitu muhimu sana katika maisha ya kiumbe chochote kile. Hivyo katika uandaaji wa chakula kumbuka kuwa na maji safi jwa ajili ya kunywa kuku wako. Maji yanakazi nyingi katika mwili wa kiumbe chochote kama vile, kupunguza joto, kurahisisha mmeng'enyo wa chakula, kulainisha kinyesi.

google+

linkedin

About Author
  • Naitwa Mordecai Minga,Karibu kwanye blog hii ya ufugaji wa kuku kibiashara zaidi Read More

    0 comments:

    POST A COMMENT

     

    mail

    Enter your email address:

    Delivered by FeedBurner