Soko ni uhitaji wa bidhaa kwa watu wanaotumia au ni mahitaji ya kila siku ya binadamu ambayo yamegawanyika katika sehemu tatu ambazo ni chakula, mavazi na maladhi. Watu wengi tunachanganya sana hapo kwenye swala la soko. Soko sio jengo au sehemu ambayo tumezoea kwenda kununua bidhaa mbalimbali.
Tukija kwenye kona yetu ya ufugaji wa kuku, ni muhimu kutazama soko linataka ni kabla ya kuanza kuanzisha mradi wako. Sasa hapo ndio pa kuwa makini sana. Soko sio kuiga kwa mwenzio anafanya nini ila ni kuangalia nini kinaitajika eneo ulipo.
Yafuatayo ni mambo 3 muhimu unayopaswa kuyajua kuhusiana na soko.
Fanya utafiti kwa kuzungukia sehemu zenye mahitaji makubwa ya bidhaa yako. Ni muhimu sana kufanya uchunguzi wa kitu unachotaka kukifanya, hii itasaidia kujua ni kwa kiasi gani bidhaa yako au wazo lako la biashara linaitajika katika sehemu uliopo. Kutambua kuwa watu wanaitaji kitu fulani ni vizuri ukafika sehemu mbalimbali ambazo bidhaa hiyo hutumika kwa wingi. Mfano, ilikujua bidhaa zitokanazo na kuku kama vile mayai na nyama n.k ni kwenye vibanda vya chips, migahawa, hotelini na migodini n.k. Hapo utajiridhisha kweli uhitaji upo au la na ni kwa kiasi gani ili uweze kujipanga namna ya kuanzisha mradi wako.
Tembelea mitandao ya kijamii, Radio, Runinga na Magazeti. Hii ni njia moja wapo ya kupata taarifa za uhitaji wa bidhaa kwa ukubwa zaidi ya eneo ulilopo na inasaidia kujipanga na kupata nguvu ya kuanza mradi au ufugaji wa faida. Kwa sasa vitu nilivyotajwa ikiwemo mitandao ya kijamii ina nafasi kubwa katika jamii kwa sasa, kwa maana watu wengi wanatumia mitandao ya kijamii na taarifa yake inasambaa kwa haraka. Hivyo kama wafugaji tunatakiwa tutazame soko kwa ukubwa.
Kutambua muhitaji au wahitaji wa bidhaa yako.Hili swala linakuja baada ya kuzungukia sehemu mbalimbali za watumiaji wa bidhaa kama yako na pia kupeluzi kwenye mitandao ya kijamii. Ndipo utambue bidhaa yako inahijika na nani hapo utakuwa umefanikiwa katika kona ya soko.
Hitimisho, soko la kuku na mayai halipo kwa mtu mmoja mmoja anayekuja nyumbani ila ni uhitaji mkubwa ambao uko sehemu ambayo bidhaa hiyo inatumika kwa wingi zaidi. Kuongezea soko la kuku ni kubwa lakini sio katika uzalishaji mdogo, hatuwezi kupata faida ndio maana wafugaji wengi wadogo hatuoni faida kulingana na gharama za uendeshaji kama vile chakula, madawa n.k. lakini ukiingia kwenye ufugaji mkubwa ambao una taarifa sahihi za uhitaji wake katika jamii, hapo ni wewe mfugaji , ndio utakutana na changamoto ya kukidhi soko ulilopata.
Nikushukuru ndugu msomaji na mfwatiliaji wa makala hizi na pia nikutakie "Heri ya Chrismas" na "Mwaka Mpya wa 2018". Bila kusahau nikukaribishe kwenye ukurasa wetu wa "kukukibiashara" katika Facebook na u "like" ilikupata taarifa za makala mpya pindi inapoingia kwenye ukurasa.
0 comments:
POST A COMMENT