1.MHARO MWEUPE
(Pullorum bacilary diarrhoea)
Ugonjwa huu huathiri zaidi vifaranga kabla ya wiki nne huharisha mharo mweupe.
TIBA: Usafi pekee kwenye banda na kuepusha maji yasimwagike ovyo
2. KIPINDUPINDU CHA KUKU
( Fowl cholera)
Kinyesi cha kuku ni njano
TIBA: Tumia dawa za salfa :- Esb3, Amprollium
3. KINYESI CHA KIJIVU
( Coccidiosis)
Mwanzo kinyesi cha kijivu na baadae huharisha damu iliyochanganyika.
TIBA: Dawa ya VITACOX au ANTICOX
4. MDONDO
(Newcastle)
Kuku hunya kinyesi cha kijani sio kila kijani ni newcastle HAKUNA TIBA
5. KINYESI CHEUPE
(Typhoid)
Kinyesi Kinagandia sehemu za nyuma au hulowana sehemu za haja
TIBA: Dawa ni Esb 3
6. GUMBORO
Huathiri zaidi vifaranga kinyesi huwa ni majimaji
TIBA: Hakuna dawa tumia vitamini na antibiotic
0 comments:
POST A COMMENT