KUKUKIBIASHARA
Breaking News
Loading...

Ad

Jumanne, 4 Septemba 2018

USINUNUE KUKU WA KUFUGA KWENYE VYANZO HIVI.


Habari, ndugu msomaji Na mfuatiliaji wa makala zetu za UFUGAJI wa Kuku. Ni matumai yetu u mzima wa afya njema Na ukotayari kutimiza majukumu yako ya kila siku. Pia tuwao.bee wenzetu walio tangulia mbele za haki Amani mana hata sisi tuko njiani kuelekea huko.
Tulejee kwenye somo letu la Leo kama linavyojieleza hapo huu. Mdau yoyote anapotaka kuanza kufuga Kuku Mara nyingi huwa anajiuliza atapata wapi Kuku hapo wa kufuga Na pia kuna sehemu nyingi sana ambazo unaweza kupata Kuku wa kufuga lakini sehemu au vyanzo hivi usinunue Kuku wako wa kufuga, navyo ni..
Sokoni ni sehemu mojawapo ambayo Kuku huuzwa kwa ajili ya watu wanaotafuta ili wasiangaike kwenda vijijini au kwa mana nyingine sokoni ni sehemu ambayo inarahisisha upatikanaji wa bidhaa kama Kuku. Sasa kwa mtu ambaye anataka kufuga Kuku kama mradi, sokoni siyo sehemu sahihi kwa sababu Mara nyingi Kuku wale huwa wanatolewa kwenye vyanzo visivyofuata taratibu za ufugaji, kwa mana unaweza nunua Kuku wako pale Na baada ya siku chache wanaanza kuugua Na kufa. Mara nyingi Kuku wale hawana chanjo Na wengine wanakuwa wagonjwa. Hivyo wewe kama mfugaji unapaswa kununua Kuku kwenye chanzo sahihi ili usijepata hasara.
Mnadani ni sehemu ambayo wafanyabiashara wanapeleka bidhaa zao Na kukuta Na wanunuzi wa bidhaa hizo. Pia kuna wafanyabiashara wa Kuku ambao Mara nyingi hukusanya Kuku kutoka vyanzo mbalimbali Na kuwaleta mnadani. Hivyo kwa mtu ambaye anataka Kuku wa kufuga mnadani sio sehemu sahihi ya kununua Kuku wa kufuga. Mana on ileile kwamba Kuku wa kufuga lazma ujue taarifa zake za nyuma kama vile kupewa chanjo Na vingine ili ujue unaanzia wapi Na pia kama katokea kwenye chanzo kizuri atakuwa hana shida yoyote, pia faida ya kununua kwenye chanzo kinachofahamika ni rahisi unapopata tatizo kurejea uliponunua nakupata ufumbuzi lakini Kuku wa mnadani ni vigumu kujua Kuku huyo katokea wapi hivyo unaweza kununua kumbe anaumwa Na baada ya kumfikisha nyumbani anakufa na itakuwa hasara.
Kwa ujumla sokoni na mnadani ni sehemu sahihi ya kupata Kuku wa kitoweo na sio wa kufuga.
Hitimisho, chanzo sahihi cha kupata Kuku wa kufuga ni kwa mfugaji ambaye anafuata taratibu zote za ufugaji kama kuwapa chanjo zote Kuku wake Na dawa ya minyio

Jumamosi, 18 Agosti 2018

Habari ndugu wadau wa kukukibiashara, tuwaombe ladhi kwa kutokuwa hewani kwa muda sasa, nikutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu pale tutakapo timiza taratibu za mtandao tutarudi hewani kama kawaida. Tunawaomba ladhi sana kwa usumbufu. Asante tunawatakia siku njema.

Jumamosi, 10 Februari 2018

Hii ni mifumo ambayo inatumika kufugia kuku Tanzania

Aina za ufugaji wa kuku
Kuna aina mbili za ufugaji wa kuku katika nchi ya Tanzania

1. UFUGAJI URIA

kuku wanajitafutia chakula wenyewe. Aina hii kuku hufungiwa bandani usiku lakini mchana hufunguliwa na kuachwa wajitafutia chakula na maji wenyewe kasha hurudi tena bandani usiku. Na ndio mfumo ambao kaya nyingi za kitamzania zinautumia.

Faida ya ufugaji uria

i. Hakuna gharama za chakula
ii. Kuku hujipatia aina mbali mbali za vyakula kama wadudu, majani na nafaka hivyo hujipatia mlo kamili.
iii. Mtaji, wake ni mdogo kwani hutumia ujenzi rahisi wa mabanda.
iv. Kuku wanaofungiwa kwa njia hii huwa na chanjo.
v. Kuku hawavunji mayai hawapigani, wala kunyonyoana manyoya.

Changamoto

i. Ni ngumu kuzuia minyoo na magonjwa.
ii. Kuku wadogo (vifaranga) huliwa na wanyama na ndege. Mayai hupotea na kuliwa na viumbe waharibifu.
iii. Kuku hupata shida ya mvua na baridi.
iv. Kuku wanaofungiwa kwa njia hii huwa na chanjo.
v. Nafasi kubwa huitajika kwa ajili ya kuwapa kuku nafasi ya kujitafutia chakula cha kutosha.

2. UFUGAJI NUSU URIA

Aina hii ya kuku hujengewa banda na uzungushiwa senyenge kuzuia kuku wasifike mbali na chakula na pia hujengewa sehemu ya kutaga mayai.

Faida

I. Ujenzi ni rahisi
ii. Mbolea usambaa kwa urahisi shambani
iii. Ni rahisi kuzuia na kukinga magonjwa.
iv. Ni rahisi kuokota mayai na pia mayai hayo hayaliwi na wanyama wasumbufu.
v. Hupungua gharama za chakula kwani kuku ujotafutia na kupewa kiasi kidogo cha nyongeza.

Kuna aina mbili za kufuga kuku wa ndani

i) battery cage system.
ii) deap litre system.

Tanzania hutumia njia deap litre system ambapo maranda ya mbao, majani ya mpunga, ngano na pumba za mchele hutumika sakafani kiasi cha 10-15 za ujazo.
- tandiko ambalo ubadilishwa mara tu linapobonyea au kuchanganyika na mbolea au kila baada ya miezi mitatu (3)
- kuku hupewa chakula, kuwekewa viota vya kutagia kuku afugwe kwa kufuata vipimo vya eneo ambavyo ni kuku 2-3 kwa 1m2
- banda hujengwa urefu wa 60 cm kwa tofali au udongo sehemu inayobaki huwa ni kwa kuruhusu mzunguko wa hewa.

Faida zake

1. Kuku wengi hufugwa katika sehemu ndogo
2. Kuku hupata kinga za hali ya hewa, mvua, jua na baridi. Pia hukingwa zaidi na wanyama wasumbufu kama mwewe, panya na nyoka.
3. Mayai hukusanywa kwa urahisi.
4. Kuku hufugwa kibiashara rahisi kukinga magonjwa na wadudu.
5. Mbolea hupatikana kwa wingi.

Changamoto

1. Chakula kisipochanganywa vizuri hakitumiki
2. Gharama kubwa hutumika kujengea banda.

Hizi ni aina za kuku wanaopatikana Tanzania

AINA ZA KUKU
kuna aina kuu mbili za kuku
1. Kuku wa asili ( kuku wa kienyeji)
2. Kuku wa kisasa

Kuku wa asili
Hawa utofautiana katika maumbo, utagaji, uzito, rangi ya manyoya, ukuaji na uwezo wa kutaga mayai. Kuku wa kienyeji hukua taratibu na utaga mayai machache.

Kuku wa kisasa (zaotic breed)
Hawa ni kuku toka nchi za kigeni pia wana aina mbili ambazo ni
i. Kuku chotara
ii. Pure breed

Kuku chotara
Ni mchanganyiko wa aina mbili au zaidi ya kuku. Siku hizi kuku wanaotakiwa kibiashara ni kuku chotara ( wengine ni wa mayai na wa nyama)

Pure breed
Hawa wanagawanyika sehemu mbili kuku (a) kuku wazito ( hutoa nyama) broiler
(b) kuku wepesi ( hutaga mayai) layers

Jumanne, 2 Januari 2018

Faida sita (6) za kutumia banda la kisasa (cage)

Karibu ndugu mfuatiliaji wa makala hizi za ufugaji wa kuku. Nimatumai yangu una afya njema ili kuweza kuwa pamoja na mimi katika kujifunza changamoto na namna ya kufanikiwa katika swala zima la ufugaji. Karibu leo katika mada nyingine inayohusu banda la kisasa ( kwa lugha ya kigeni inaitwa "cage") ambalo inafaida nyingi nzuri katika kupunguza changamoto mbalimbali za ufugaji wa kuku. Cage imeleta utofauti mkubwa japo ni gharama lakini ukitazama kwa jicho la tofauti au kwa kina utagundua ufugaji wa kawaida una changamoto nyingi ambazo zinaweza pelekea kufikia gharama za kuwa na cage.

Zifuatazo ni faida za kutumia cage (banda la kisasa)

1.kuzuia upotevu wa chakula. Banda hii limetengenezwa katika ubora ambao unawezesha kuku kupata nafasi ya kutoa kichwa nje ya banda na kula chakula chake bila kuchakua na mdomo au miguu ambayo mara nyingi ndio inayosababisha umwagaji wa chakula chini na kupelekea upotevu wa chakula kingi chini. Namna inavyokuwa ni kwamba kuku anakuwa kwa ndani lakini sehemu ya chakula ipo kwa nje.

2. Unatumia muda mchache kuhudumia kuku wengi. Hii ni faida nyingine ya banda hili la kisasa maana hapa tunaweza kuzungumzia ufugaji mkubwa wa kuku kuanzia kuku 200 na kuendelea. Namna ya kuwa hudumia wakiwa chini katika banda la kawaida ni changamoto, kwa namna ya kuwapa chakula, kuokota mayai kama ni kuku wa mayai, kusafisha banda n.k lakini matumizi ya cage hurahisisha namna zote kwa maana ulishaji wa chakula, kuokota mayai na kusafisha banda kwa urahisi ndani ya muda mfupi unaweza kuhudumia kuku zaidi ya 1000.

3. Hupunguza magonjwa ya kuambukizwa. Katika mabanda yetu ya kawaida kwa maana ya chumba ambacho kuku wanakuwa chini mara nyingi, kuku hula kinyesi chake au cha mwingine kulingana na eneo husika. Hivyo ni rahisi sana kwa kuku mgonjwa kuweza kuambukiza kuku wengine hasa kupitia kinyesi. Lakini hii ni tofauti ukitumia cage, kinyesi chote kinadondokea chini bila kufika katika sehemu nyingine ambapo kuku wapo.

4. Kujua idadi kamili. Kwa kawaida kuku wanaofugwa chini ni vigumu sana kuweza kuwa hssabu na kujua idadi kamili hasa kuanzia kuku mia na kuendelea na pia hata kama kuna wizi unafanyika kugundua si rahisi, lakini matumizi ya cage hurahisisha kuwa na takrimu sahihi za kuku wako, kwa sababu cage moja inakaa kuku 96 na ndani yake kuna visehemu ambavyo hukaa kuku wa 4 kila kisehemu. Hivyo ni rahisi kujua idadi ya kuku wako kila siku.

5. Inarahisisha zoezi la ukusanyaji wa mayai. Namna cage ilivyotengenezwa inaruhusu kuku kutaga na yai kushuka toka ndani na kuja nje ya banda ambapo kuna sehemu maalumu kwa ajili ya mayai yaliyotagwa ilikukusanywa kirahisi, tofauti na utaratibu wa kawaida tuliouzoea kuokota mayai chini. Ambapo muda mwingine kama kuku wana upungufu wa madini ya calcium hula mayai yake lakini kwenye banda hili hawezi fanikiwa kula yai kwa namna banda lilivyotengenezwa.

6. Inarahisisha kusafisha na kukusanya mbolea. Hili zoezi liko kama ifuatavyo, banda hili lina ngazi tatu kwa namna lilivyotengenezwa katika pande zote kushoto na kulia ila kila sehemu ya banda ambapo kuku hukaa ina uwazi wa kudondosha kinyesi chini bila kuangukia kwa wengine na kwa namna banda lilivyo kinyesi chote kitakuwa chini ambapo kuna uwazi mkubwa wa kuruhusu mfugaji kuweza kusafisha kwa urahisi na kuku sanya mboleo.

Himisho kwa faida za kuwa na zao bora la mradi wako. Tunashauriwa ni vyema tukatumia banda la kisasa. Lina matokeo mazuri zaidi, japo ni gharama lakini ubora wake ni maradufu ya ufugaji wa kawaida. Changamoto nyingi zinapungua katika matumizi ya cage ( banda la kisasa ). Napenda kuchukua fursa hii kukushukuru ndugu msomaji na mfuatiliaji kwa kuwa pamoja na mimi kuanzia mwanzo wa makala hadi kufikia hapa. Karibu tena katika mfululizo wa makala zijazo siku kama ya leo.

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

Jumatatu, 1 Januari 2018

Hizi ni faida za ufugaji wa kuku kama fursa

Fursa katika ufugaji wa kuku
Fursa ni changamoto au matatizo yaliyotuzunguka. Kwa maana nyingine ni vitu gani tunavipata kwa shida kati mazingira yetu ya kawaida katika pilika za kila siku na ndio mahitaji yetu. Hiyo ni fursa. Timekuwa tukipata shida jinsi ya kujua fursa zilizotuzunguka kutokana na kutojua neno fursa lina maana gani hasa kwa mapana yake. Tukija katika kona ya ufugaji wa kuku, fursa iliyopo ni changamoto tunazokumbana nazo kila siku katika ufugaji wa kuku aina zote. Tusilalamike tuu kuwa hatuwezi fanikiwa. Kayika mazingira yetu kuku kazoeleka kama utamaduni wa kila kaya ya kitanzania kuwa na kuku lakini anachukuliwa kama mfugo wa kawaida asiye na faida yoyote ile kuku ni fursa kubwa ambayo imeqatoa watu wengi kiuchumi. Tutumie nafasi tuliyonayo kujikwamua kiuchumi.
Hizi ni faida za ufugaji wa kuku kama fursa
Kuanza na mtaji mdogo. Hii ni moja kati ya faida za kuanzisha mradi wa kuku. Kqa kawaida mtu yoyote anaweza kuanzisha mradi huu wa kuku kwa sababu hauhitaji mtaji mkubwa ili kuanza. Mfano kuku mmoja ambaye ni mtetea ma jogoo mmoja unaweza kuanza kama mradi. Changanuo ufuatao unaonyesha ni kwa jinsi gani. Mtetea mmoja na jogoo unaweza kununua kwa elfu 25 kwa maana jogoo elfu 15 na mtetea 10, baada ya mwezi mtetea atakuwa ameanza kutaga na ndani ya mwezi. Kipindi amemaliza kutaga ukamuwekea mayai 10 na 15 ndani ya siku 21 atatotoa vyote au 10. Vifaranga 10 ukowa lea mpaka miezi 6 watakuwa kuku wakubwa na baadaya hapo wataanza kutaga na kulalia na kupata vifaranga wengi na ukaendelea kupata kuju wengi zaidI. Ndio maana unaweza kutumia mtaji mdogo na baada ya kuwa na kuku wengi na kuanza kuuza.
Chanzo chan mapato. Kuku ana bidhaa muhimu kama vile kuku, mayai,  nyama, na kinyeji. Vyote hivi ni mahitaji ya binadamu katika maisha ya kila siku. kupitia kufuga Kuku utapata fursa ya kutengeneza pesa nyingi tu. Kama utakuwa mfuatiliaji makini, kwa maana kuwapa chanjo kwa wakati, chakula bora na kutibu magonjwa pindi yakitokea. Kuku wa kienyeji aliyekoma anauzwa 15000, 20000, 25000, 30000 na kuendelea inategemeana na kuku mwenyewe. Tatizo kubwa tulilonalo Watanzania hasa kwa kuku wa kienyeji kadhalaulika na kuonekana ni wa kawaida lakini tukikaa kujua trei moja mayai ya kienyeji linauzwa 15000. Je? Ukiwa unaweza kuzalisha trai 5 kwa siku utakuwa na shilingi ngapi. Tuamke na kufanya ufugaji wa kuku kuwa wa uwakika.
Utawala wa mradi wa kuku ni rahisi. Urahisi huu hauna maana kuwa hakuna ugumu hapana ila maana kubwa ya hii pointi ni kwamba hatakama ni mfanyakazi wa kuajiliwa utapata muda wa kufuatilia kwa karibu maendeleo ya kuku wako. Mfano umeanza na mradi wako wa kuku 100 ,umewafugia nyumbani kwa kawaida unatakiwa kujipangia ratiba. Kwamba kabla ya kwenda kazi ni kufika bandani na kuwa hudumia kuku wako, hata kama utamwachia kijana aendelee kuwa hudumia kipindi ukiwa kazini, utakuwa unajua kuku wako wako salama. Pia jioni ukitoka kazini inabidi upate muda wa kipitia bandani na kuona hali ilivyo na kupata mrejesho kutoka kwa kijana uliyemwachia.
Soko la kuku ni kubwa Tanzania na nchi za nje pia.Hili swala ni fursa kubwa kwetu sisi vijana hasa ambao tumekuwa tukilalamikia ishu ya ajira za serikali na mashirika binafsi. Lakini tazama watu wa nje ya nchi na baadhi ya wenyeji wanaoingiza bidhaa za kuku kama, vifaranga, kuku na mayai. Wakati nafasi ya kuzalisha hapa hapa tunayo ni swala la maamuzi na kuacha kulalamikia serikali juu ya ajira. Vijana ajira tunayo mikononi mwetu ni swala la kuchukua hatua. Uwezekano upo kwa Tanzania kuanza kujihidumia yenyewe na kuanza kutoka nje ya mipaka pia. Takrimu zinaonyesha bado hata nusu ya matumizi ya kuku kwa ndani ya nchi, Cha msingi ni sisi kutafuta taarifa sahihi ili kuweza kufanya maamuzi sahihi. mojawapo ya chanzo kizuri cha taarifa za kilimo na ufugaji ni ESRF na youtube tazama knowledge tv.
Mradi wa kuku ni benki hai. Benki hai ni namna ya kuhifadhi pesa yako kwa matumizi ya baadae. Sasa ufugaji wa kuku ni benki hai maana yake ukiwekeza pesa yako katika kuku itakuwa sehemu salama na itaongezeka kwa kadri unavyozidi kuzalisha kuku wengi. Benki hii ni tofauti na benki za kawaida kwa sababu hakuna gharama yoyote ya makato ya uendeshaji, hapa ni kuhakikisha pesa yako inakuwa ni jitihada zako kuhakikisha unazalisha kuku wengi.
Nikutakie kila la heri kwenye kuazimisha mwaka mpya wa 2018 wenye mafanikio makubwa ya malengo yako na watu waliokuzunguka. Karibu sana katika ukurasa wetu facebook na kwenye whatsapp group ili uweze kujumuika na wafugaji wengine kubadilishana uzoefu na mafundisho mbalimbali kutoka kwa wataalamu waliobobea katika ufugaji wa kuki kisasa.

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

Jumanne, 26 Desemba 2017

Mambo matatu (3) muhimu unayopaswa kuyajua kuhusiana na soko.

Soko ni uhitaji wa bidhaa kwa watu wanaotumia au ni mahitaji ya kila siku ya binadamu ambayo yamegawanyika katika sehemu tatu ambazo ni chakula, mavazi na maladhi. Watu wengi tunachanganya sana hapo kwenye swala la soko. Soko sio jengo au sehemu ambayo tumezoea kwenda kununua bidhaa mbalimbali.

Tukija kwenye kona yetu ya ufugaji wa kuku, ni muhimu kutazama soko linataka ni kabla ya kuanza kuanzisha mradi wako. Sasa hapo ndio pa kuwa makini sana. Soko sio kuiga kwa mwenzio anafanya nini ila ni kuangalia nini kinaitajika eneo ulipo.

Yafuatayo ni mambo 3 muhimu unayopaswa kuyajua kuhusiana na soko.

Fanya utafiti kwa kuzungukia sehemu zenye mahitaji makubwa ya bidhaa yako. Ni muhimu sana kufanya uchunguzi wa kitu unachotaka kukifanya, hii itasaidia kujua ni kwa kiasi gani bidhaa yako au wazo lako la biashara linaitajika katika sehemu uliopo. Kutambua kuwa watu wanaitaji kitu fulani ni vizuri ukafika sehemu mbalimbali ambazo bidhaa hiyo hutumika kwa wingi. Mfano, ilikujua bidhaa zitokanazo na kuku kama vile mayai na nyama n.k ni kwenye vibanda vya chips, migahawa, hotelini na migodini n.k. Hapo utajiridhisha kweli uhitaji upo au la na ni kwa kiasi gani ili uweze kujipanga namna ya kuanzisha mradi wako.

Tembelea mitandao ya kijamii, Radio, Runinga na Magazeti. Hii ni njia moja wapo ya kupata taarifa za uhitaji wa bidhaa kwa ukubwa zaidi ya eneo ulilopo na inasaidia kujipanga na kupata nguvu ya kuanza mradi au ufugaji wa faida. Kwa sasa vitu nilivyotajwa ikiwemo mitandao ya kijamii ina nafasi kubwa katika jamii kwa sasa, kwa maana watu wengi wanatumia mitandao ya kijamii na taarifa yake inasambaa kwa haraka. Hivyo kama wafugaji tunatakiwa tutazame soko kwa ukubwa.

Kutambua muhitaji au wahitaji wa bidhaa yako.Hili swala linakuja baada ya kuzungukia sehemu mbalimbali za watumiaji wa bidhaa kama yako na pia kupeluzi kwenye mitandao ya kijamii. Ndipo utambue bidhaa yako inahijika na nani hapo utakuwa umefanikiwa katika kona ya soko.

Hitimisho, soko la kuku na mayai halipo kwa mtu mmoja mmoja anayekuja nyumbani ila ni uhitaji mkubwa ambao uko sehemu ambayo bidhaa hiyo inatumika kwa wingi zaidi. Kuongezea soko la kuku ni kubwa lakini sio katika uzalishaji mdogo, hatuwezi kupata faida ndio maana wafugaji wengi wadogo hatuoni faida kulingana na gharama za uendeshaji kama vile chakula, madawa n.k. lakini ukiingia kwenye ufugaji mkubwa ambao una taarifa sahihi za uhitaji wake katika jamii, hapo ni wewe mfugaji , ndio utakutana na changamoto ya kukidhi soko ulilopata.
Nikushukuru ndugu msomaji na mfwatiliaji wa makala hizi na pia nikutakie "Heri ya Chrismas" na "Mwaka Mpya wa 2018". Bila kusahau nikukaribishe kwenye ukurasa wetu wa "kukukibiashara" katika Facebook na u "like" ilikupata taarifa za makala mpya pindi inapoingia kwenye ukurasa.

Jumapili, 10 Desemba 2017

Vitu vitano (5) vya muhimu kuweka kwenye chakula cha kuku

Habari ndugu msomaji na mfuatiliaji wa blog hii, karibu tena tuweze kuelimishana kwa kupata maarifa zaidi na jinsi ya kupambana na changamoto za ufugaji kiujumla ili tuweze kutumia fursa hii ya Tanzania ya viwanda na kuweza kuhudumia kitoweo badala kuwaachia wachache waagize nje ya nchi, wakati wazawa tunazalisha pia.
Niingie moja kwa moja kwenye mada yetu ya leo kuhusu vitu muhimu vinavyotakiwa kwenye chakula cha kuku.Kuna vitu vitano muhimu vinavyotaijika kwa kuku ili awe na afya bora. Navyo ni kama vifuatavyo.

1. Protini.
2. Mafuta.
3. Wanga.
4. Madini.
5. Vitamini.

1.PROTINI
Ni aina ya vyakula ambavyo kazi yake kubwa ni kukuza mwili navyo ni kama ifuatavyo,
-Mtama, Dagaa, Alizeti na Soya
Hivi vyote inategemeana na maeneo uliko, nini kinapatikana kwa urahisi.

2. WANGA.
Ni aina ya vyakula ambavyo kazi yake ni kuupa mwili nguvu. Navyo ni kama ifuatavyo
-mahindi yaliyo balazwa
-pumba ya mahindi
-pumba ya mpunga

3. MAFUTA.
Ni aina ya vyakula ambavyo kazi yake kubwa ni kuupa mwili joto pamoja na kulainisha mmeng'enyo wa chakula mwilini. Kundi hili kuna vitu vifuatavyo
- mashudu ya alizeti
- mashudu ya pamba

4. MADINI
Hapa kuna madini ya aina mbalimbali ambayo kazi yake kubwa ni kuimarisha mifupa na ganda la juu la yai pia. Na haya madini ni muhimu sana, kwa sababu yanakazi kubwa katika mwili wa kuku. Yanamwezesha kuku kutembea vizuri na kwa ukakamavu. Pia yai la kuku ili liwe imara lenye ganda gumu lazima apate madini ya kutosha. Bila kusahau madini yanasaidia kuku kutonyonyoka manyoya yake. Madini hayo ni kama ifuatavyo,
- Mifupa
- Chokaa ya kuku
- D.C.P - Dicalcium Phosphate. ( hizuia kudonoana, kula mayai, maganda malaini. Pia huimarisha maganda ya mayai, husaidia kuongeza mayai )

5. VITAMINI.
Ni aina ya vyakula ambavyo vinapatikana sana kwenye mbogmboga n.k lakini kazi yake kubwa ni kuimarisha mwili uwe vizuri kama vile kuona, kuwa na manyoya imara na afya bora. Kundi hili linavyakula kama vifuatavyo
- mchicha
- chainizi
- spinachi
- majani ya paipai

KUMBUKA:
Pia katika maduka ya mifugo kuna vitamini zinauzwa ambazo hutumika pia kama mbadala wa mazingira yetu yalivyo kuna baadhi ya maeneo kupata mbogamboga ni changamoto. Kuna "vitalyte" ni nzuri kwa kuku na hata nyingine pia.

Pia kuna kitu kingine vya msingi katika chakula cha kuku.

PREMIX
Ni aina ya virutubisho amabvyo hutumika kulingana na aina ya kuku. Inaleta matokeo chanya kwa kuku Muda mwingine huitwa busta. Nazo zipo katika mahindi mawili ambazo ni..
1. Layers concentrate
2. Broiler concentrate

MAJI.
Maji ni kitu muhimu sana katika maisha ya kiumbe chochote kile. Hivyo katika uandaaji wa chakula kumbuka kuwa na maji safi jwa ajili ya kunywa kuku wako. Maji yanakazi nyingi katika mwili wa kiumbe chochote kama vile, kupunguza joto, kurahisisha mmeng'enyo wa chakula, kulainisha kinyesi.

Jumapili, 3 Desemba 2017

MAMBO SITA (6) YA KUHAKIKISHA UZAO WA KUKU WAKO

Karibu sana ndugu msomaji na mfuatiliaji wa makala hizi za ufugaji wa kuku aina zote kulingana na fursa tuliyonayo katika nchi yetu. Nimatumai ya kwamba u mzima wa afya
Karibu katika mada ya leo ambayo itakusaidia kuweza kutatua changamoto ya kuweza kuwa na kuku wengi kwa kadri, Mungu atavyo kujalia uhai.
Mada yetu ya leo inahusu izao wa uhakika wa kuku wako bila kubahatisha. Hasa kwa wafugaji wa kuku wa kienyeji majumbani kwetu. Tumekuwa na mazoea ya kumwachia kuku ajilee mwenyewe na kutarajia kupata kitu bora. Katika uharisia haiwezekanai. Ufwatiliaji wa karibu ni muhimu ili kujihakikishia angalai asilimia 80 hadi 90 ya kufanikisha kile unachokitaka.
Yafuatayo ni mambo sita (6) ya kuhakikisha uzao wa kuku wako
1. Kuchukua mayai kila yanapotagwa.
Kuku pindi atakapofikia kuanza kutaga mayai, ni muda muafaka kuanza zoezi hili la hatua ya kwanza lakini subiri atakapo taga mayai mawili hadi matatu ndipo uanze kuchukua na hapo naomba tuelewane kwamba, kuku wako akifikisha mayai mawili itakuwa na maana ni siku yake ya pili kutaga. Kuku kwa kawaida hasa wa kienyeji hutaga yai moja kwa siku. Hivyo zoezi la kuchukua mayai ni pale atakapotaga yai la tatu ndipo uchukue na kuacha yale mawili yaliyotangulia kutagwa. Ni muhimu sana kuchukua yai jipya.
2. Kuweka alama katika kila yai .
uwekaji wa alama katika mayai ni muhimu sana ili kuweza kutambua yai limetagwa lini na kwa pendekezo hakikisha una kalamu ya mkaa (penseli) na uweke alama ya namba ( kama vile 1, 2, 3,.......) hii itasaidia kujua ni yai la ngapi kutagwa tangu kuku wako aanze kutaga. Kabla ya kuweka alama hakikisha mikono yako haina harufu yoyote ile, hivyo kama mikono yako ina harufu, chukua majivu yanawe kama maji, yatakusaidia kuondoa harufu. Andika namba kwenye yai moja kila linapotagwa kwa kuanza na namba moja na kuendelea.
3. Kuhifadhi sehemu salama.
Baadaya kuchukua na kuweka alama hakikisha umeanda sehemu nzuri ambayo haina joto na watoto hawawezi kuchezea. Sehemu hiyo inaweza kuwa kwenye treyi lako au boxi ambalo umeweka malanda ya mbao au pumba ya mpunga na kuyapanga vizuri kulingana na namba ulizo weka kama alama na kimsingi utakuwa umeanza na yai la tatu tangu kutagwa. Hakikisha sehemu uliyoweka hakuna joto maana yai likipata joto litaharibika.
4. Kuchuka mayai yasiyozidi wiki mbili kwa ajili ya kuatamiwa.
Yai bora kwa ajili ya kuatamiwa ni lile lisilozidi wiki mbili tangu kutagwa. Katika zoezi hili hakikisha unachukua mayai yote uliyoyahifadhi. Kuku aliye vizuri katika utagaji hutaga mayai kumi na tano hadi ishirini, hivyo kwa kuwa uliweka alama katika mayai uliyo ya hifadhi anzia namba ya mwisho kuandikwa kurudi nyuma,kwa maana anza na yai la mwisho kutagwa kurudi nyuma lakini hakikisha unakumbukumbu ya tarehe ya kuku alipoanza kutaga, hiyo itakusaidia kujua mayai ya wiki mbili tangu kutagwa ni yapi. Muwekee kuku mayai 12 hadi 15 kulingana na umbo la kuku wako. Mfano kuku wako kataga mayai 15, hivyo utachukua yai la 15 hadi namba ya yai itakalo kuwa ndani ya muda unaofaa. Kuku wa kienyeji hutagi siku zote mfululizo kuna baadhi ya siku anaruka kwa hiyo hayo mayai kumi na tano yanaweza kuwa yametagwa kwa wiki tatu.
5. Siku ya kumi baada ya kuatamiwa, yapime mayai.
Hii ni sehemu au zoezi muhimu sana ilikuweza kujua kuwa mayai yaliyoatamiwa yatafaa au la. Upimaji hufanyika usiku kwa maana giza likiingia ambapo kuku wote watakuwa bandani. Zoezi hili linaitaji watu wawili ili kuweza kufanikisha. Mmoja kumshika kuku na mwingine kufanya zoezi la upimaji.Chukua tochi, mikono ya mpimaji isiwe na harufu, hivyo kujiridhisha kwa kunawa majivu na kuanza zoezi la upimaji. Chukua yai mojamoja, halafu kiganja chako kimoja kitengeneze umbo la sifuri kwa kutumia kidole gumba na kidole kinachofuatia baada ya hapo weka yai kwa juu yake kwa kutanguliza sehemu iliyochongoka iwe chini. Halafu chukua tochi na murika kwa chini kule kulikochongoka yai, utaona mambo mawili kwanza, kama yai ni zima utaona kitu cheusi ndani ya yai ujue linafaa kuendelea kuatamiwa. Pili, kama utaona yai ni jeupe ( transparent) ujue ilo yai halifai kwa kutotolewa. Zoezi litaendelea mpaka mayai yote yaishe hapo utakuwa umejihakikishia kuwa ni mayai mangapi mazima na yatatotolewa.
6.kutotolewa kwa mayai yote yaliyoatamiwa
Mpaka kufika hapo zoezi zima litakuwa limefanikiwa kwa asilimia 90 hadi 100 kwa maana ya kutotolewa vifaranga vyote ambavyo katika upimaji utakuwa umejiridhisha kuwa ni mayai mangapi yatatotolewa na ni uhakika idadi iyo iyo ya upimaji kufika katika utotolewaji.
Hitimisho, nipende kusisitiza kuwa katika zoezi zima la hatua ya kwanza hadi ya mwisho mayai yako yawe yamewekwa kwa kutanguliza sehemu iliyochongoka chini na pana juu hasa kwenye hatua ya kuhifadhi pindi unapoyachukua yanapotagwa. Nikushukuru ndugu msomaji kwa kuwa nami tangu hatua ya kwanza hadi ya mwisho. Hakiki utakuwa umepata kitu na kukifanyia kazi. Karibu sana tena katika makala zinazofuata

Jumatatu, 27 Novemba 2017

Ni kwanini kuku wako anakufa bila kujua?

Nimatumaini yangu ndugu msomaji, u mzima wa afya njema kwa kadri Mungu alivyokujalia kuamka salama. Ni muhimu kwangu kuhakikisha unapata taaeifa sahihi kuhusiana na ufugaji wa kuku aina zote. Leo nimependa kukuletea somo muhimu sana kwako kama linavyojieleza hapo juu.
Niingie moja kwa moja kwenye somo la leo, kuku ni ndege mchangamfu sana katika ubora wa afya yake. Mara nyingi kuku akiwa anaumwa kuna dalili mbalimbali atazionyesha ili kama mfugaji ukiwa makini ni rahisi kutambua na kumsaidia au kumtibu.

Zifuatazo ni dalili mbalimbali ambazo utaziona kwa kuku wako ili ujue ni ugonjwa gani.

1.Kuku kuzubaa ni moja ya dalili isiyo ya kawaida kwa kuku. Mara zote kuku ni mchangamfu sana kufikia kwamba hawezi tulia sehemu moja. Kwa hiyo ukiona kuku wako amezubaa kwa muda mrefu ujue kuna tatizo, hivyo ni muhimu kuchunguza tatizo ni nini ili uweze kumtibu kwa wakati kabla madhara makubwa kutokea. Mfano, siku moja nilikuta kuku wangu kazubaa. Ikabidi nimfuatie kwa muda lakini sikufanikiwa kugundua chochote au tatizo, maana sikuwa nae muda mwingi. Ikabidi nifanye maamuzi ya kumchinja, nilichokikuta ndani ya tumbo la kuku huyo ni utumbo pamoja na firigisi vimeoza japokuwa kuku alikuwa hai kabla ya kuchinjwa.

2.Kujitenga kwa kuku ni tabia ya tofauti kabisa kwa kuku. Kuku hupenda kukaa pamoja na wenzie muda mwingi wakicheza na kula chakula pamoja na wenzie ndio sifa yake. Kujitenga maana hanafuraha yoyote ya kushiriki na wenzie. Kimsingi hapo utakuta anasumbuliwa na mafua na kukaa pembeni. Muda mwingine unaweza mshika na asishituke kabisa. Hapo mfugaji chukua hatua.

3. Kushusha mabawa ni dalili nyingine ambayo kuku huonyesha pale ambapo hayuko sawa kiafya. Kuku mwenye afya njema mabawa pamoja na mkia wake vinakuwa juu na kucheza cheza kuashiria kuwa anafuraha na afya njema kabisa. Mtazame kuku wako takribani dakika 15 hadi 30 kwa siku ilikufuatilia kama wako salama.

4. Rangi ya kinyesi cha kuku ni mojawapo ya dalili muhimu sana katika ufugaji bora wa kuku wako. Kuku mwenye afya njema hijisaidia kinyesi cha rangi nyeusi na mara nyingine. Imechanganyika na kijani kidogo. Hivyo tofauti na rangi hizo, rangi nyingine huashiria magonjwa mbalimbali. Mfano, kuna kinyesi cha rangi ya njano, nyeupe, brown, kijivu na kijani tupu.

5. Kukosa hamu ya kula ni mojawapo ya dalili muhimu kujua na kwa leo itakuwa dalili ya mwisho katika zilizoorodheshwa lakini sio ya mwisho kabisa zipo nyingine nyingi sana. Kuku kwa tabia yao hupenda kula muda wote ni mara chache sana kukuta ametulia au kupumzika kula.hivyo ukiona umekaa dakika 15 hadi 30, kuku hali chochote hapo kuna tatizo ni vyema ukachukua hatua.

Tunawajibika kufanya yafuatayo kwa ajili ya kuboresha ufugaji wetu.

Kuwafuatilia kuku wako kwa karibu. Holi jambo ni muhimu sana kwa mfugaji na pia ni wajibu kama unatarajia zao bora. Jiwekee muda fulani kwa siku takribani saa nzima kukaa ukiwaangalia kuku wako na kuona kama wanaendeleaje? Kuna tabia ya wafugaji wengi kuwa achia vijana wao wa kazi au vibarua kufuatilia mifugo yake na yeye kusimamia kwa simu na kubaki kuwa mtu wa kupewa ripoti. Hili jambo haliwezi kuleta mazao chanya na bora, pata muda wa kufuatilia kwa karibu ili kama kuna tatizo utagundua tu kirahisi na kulifanyia kazi.

Lingine ni kuwa wa kwanza kufika bandani asubuhi kabla ya kuwafungulia kuku wako nje. Jambo hili ni muhimu sana kwa mfugaji. Maana utagundua mambo mengi yatakayo kusaidia katika ufugaji wako. Mfano, ni muhimu kuangalia kinyesi cha kuku walichojisaidia usiku kuamkia siku hiyo. Pia kutazama kuku wako wamechangamka n.k

Napenda kukushukuru ndugu msomaji wa makala hii kwa kuwa nami tangu mwanzo wa makala hii hadi kufikia hapa. Nimatumai yangu utakuwa umejifunza kitu. Karibu sana kuendelea kujifunza katika makala zijazo siku kama hii wiki ijayo. Asanteni

Jumapili, 26 Novemba 2017

Vifaranga wa kienyeji kabisa

https://youtu.be/k-BYOqoLCoY

Ijumaa, 3 Novemba 2017

MCHANGANUO WA CHAKULA KULINGANA NA UMRI

MCHANGANUO WA CHAKULA KULINGANA NA UMRI

UMRI (WIKI)AINA YA CHAKULA
0-2Super starter
3-8Chick starter
9-20Grower mash
21-89Layer mash

UMRI WA WIKI 1-2 (SUPER STARTER)

Wiki ya 1: gramu 12 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 2: gramu 22 kwa kuku mmoja kwa siku moja

UMRI WA WIKI 3-8 (CHICK STARTER)

Wiki ya 3: gramu 27 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 4 gramu 32 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 5: gramu 38 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 6: gramu 42 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 7: gramu 46 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 8: gramu 50 kwa kuku mmoja kwa siku moja

UMRI WA WIKI 9-18 (GROWER MASH)

Wiki ya 9: gramu 56 kwa  kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 10: gramu 62 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 11: gramu 64 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 12: gramu 66 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 13: gramu 68 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 14: gramu 74 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 15: gramu 74 kwa  kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 16: gramu 80 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 17: gramu 82 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya18: gramu 88 kwa kuku mmoja kwa siku moja

UMRI WA WIKI 19-40 (LAYERS MASH 1)

Wiki ya 19: gramu 92 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 20: gramu 102 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 21: gramu 108 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 22: gramu 114 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 23: gramu 116 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 24: gramu 120 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 25-40: gramu 130 kwa kuku mmoja kwa siku moja

UMRI WA WIKI 41-80 (LAYERS MASH 2)

Gram 130 kwa kuku mmoja kwa siku


NB: jinsi ya kubadili gramu kuwa kilo ni kama ifuatavyo
         Kilo 1 = gramu 1000
      Mfano -    una vifaranga 100 na unatakiwa kuwapa chakula cha wiki ya kwanza tangu kuzaliwa
                      kifaranga 1     = gram 12 (siku)
                      vifaranga 100 =    ?

                     vifaranga  100 kuzisha gramu 12
                                        kifaranga1
12× 100 = 1200 gramu kwa siku

Kubadili gramu 1200 kuwa kilogramu

Kilo 1 = gramu 1000
   ?     =  gramu 1200

Kilo 1 × gramu 1200
      Gramu 1000

= kilo 1.2 (kilo 1 na gramu 200) kwa kuku 100 kwa siku

Ijumaa, 22 Septemba 2017

UTAMBUZI WA MAGONJWA YA KUKU KUPITIA RANGI YA KINYESI

1.MHARO MWEUPE
   (Pullorum bacilary diarrhoea)

Ugonjwa huu huathiri zaidi vifaranga kabla ya wiki nne huharisha mharo mweupe.

TIBA: Usafi pekee kwenye banda na kuepusha maji yasimwagike ovyo

2. KIPINDUPINDU CHA KUKU
     ( Fowl cholera)

Kinyesi cha kuku ni njano

TIBA: Tumia dawa za salfa :- Esb3, Amprollium

3. KINYESI CHA KIJIVU
     ( Coccidiosis)

Mwanzo kinyesi cha kijivu na baadae huharisha damu iliyochanganyika.

TIBA: Dawa ya VITACOX au ANTICOX

4. MDONDO
     (Newcastle)

Kuku hunya kinyesi cha kijani sio kila kijani ni newcastle HAKUNA TIBA

5. KINYESI CHEUPE
     (Typhoid)

Kinyesi Kinagandia sehemu za nyuma au hulowana sehemu za haja

TIBA: Dawa ni Esb 3

6. GUMBORO

Huathiri zaidi vifaranga kinyesi huwa ni majimaji

TIBA: Hakuna dawa tumia vitamini na antibiotic

Jumamosi, 19 Agosti 2017

Vifuatavyo ni vitu ambavyo havifai kwa kuju wako kula

VITU AMBAVYO HUTAKIWI KURUHUSU KUKU WAKO WALE.

Habari ndugu msomaji wa makala za ufugaji wa kuku. Kutokana na changamoto iliyokuwa imejitokeza hatukuweza weka makala mpya lakini sasa hivi tunaendelea kama kawaida. Kuna baadhi ya vitu havifai kuwapa kuku kwa mazoea au tunawaachia tu tunapoona wanakula lakini ukweli vinakuwa na madhara

VITUNGUU ni mojawapo ya vitu ambavyo havitakiwi kwa kuku kula.vitunguu vina sumu iitwayo thiosulphate ambayo huua seli hai nyekundu. Iwapo utalisha kwa kiwango kikubwa itasababisha upungufu wa damu(anaemia) au kifo.

MAHARAGWE MABICHI AU YASIYOPIKWA ni kitu kingine ambacho hupaswi kuwapa kuku wako. Maharagwe mabichi au yasiyopikwa yana sumu iitwayo hemaglutin ambayo ni hatari kwa kuku kwahiyo unashauriwa kupika au kuchemsha kuondoa sumu hii.

MCHELE MKAVU. Tumezoea kuwapa kuku wetu kama chakula pale unapokuwa umeishiwa pumba.Kuku wanaolishwa Mchele mkavu kuna hatari mchele huo kujikusanya tumboni na kusababisha matatizo.

MAGANDA YA PARACHICHI
Kuku wanapokula maganda ya parachichi itapelekea kuingiza sumu mwilini kwa hiyo epuka maganda ya parachichi yasije kujichanganya na chakula.

MBEGU ZA APPLE
Mbegu za apple zina sumu iitwayo cyanide japokuwa kuku wanapenda apples hakikisha unatoa mbegu.

VYAKULA VYENYE CHUMVI NYINGI.
Vyakula vyenye chumvi nyingi husababisha ugonjwa uitwao hypernatremia kwa hiyo mwili wa kuku hauhitaji kiasi kikubwa cha chumvi. Kuku wanaweza kuvumilia kiasi kidogo cha chumvi nacho ni 0.25% kwenye maji. Endapo kutakuwa na uhaba inaweza kupelekea ugonjwa huo.

WADUDU WASUMBUFU KATIKA UFUGAJI WA KUKU ( VIROBOTO, CHAWA NA UTITIRI)

Mara nyingi wafugaji wanakabiliwa na changamoto kadhaa katika ufugaji wao wa kuku. Changamoto hizo ni  pamoja na wadudu wasumbufu mbalimbali mfano,  Viroboto, Utitiri na chawa. wadudu hawa wamekuwa tishio kubwa katika kufanya ufugaji wa kuku uwe wenye tija kutokana na kusababisha vifo vingi.

Katika banda lako la kuku ukivamiwa na wadudu hawa kwa hakika afya ya kuku wako itaanza kuzorota kwa haraka na kuwafanya kuku wako waonekane kama wanaumwa vile. Ni wadudu wanaonyonya damu kwa kiasi kikubwa sana na hivyo kusababisha kuku kufa kwa ugonjwa wa kuishiwa damu mwilini.

Lakini vilevile kwa kuku wanaotaga huwafanya washushe utagaji wao ghafla. Ukiwatazama unaweza kuona kama wanaumwa kwa maana wanakonda, kuzubaa na kupoteza hamu ya kula. Muda mwingi wanakuwa wanajichokonoa na kujikuna katika manyoya yao kwa kutumia midomo yao. Hii ni kutokana na adha wanayopata hasa kuwashwa na maumivu wanayosababishiwa.

Viroboto ni rahisi kuonekana kwa kuwa wanakaa sehemu za wazi za kuku mfano kuzunguka maeneo ya macho,  katika ndevu na mapanga yao nk. Tatizo ni kwa utitiri na chawa wenyewe si rahisi kuonekana kama mfugaji siyo mfuatiliaji wa karibu wa kuku wake.  Utitiri na chawa wenyewe wanakaa ndani ya manyoya ya kuku kwenye ngozi kabisa.

Utitiri ni mdogo kuliko chawa. Chawa wanakuwa weupe hivi wanajishika katika ngozi. Utawaona endapo utapekenyua katika manyoya ya kuku. Wakati utitiri wenyewe unatakiwa uwe na macho mazuri kuweza kuwaona kwa kuwa ni wadudu wadogo zaidi lakini ukipekenyua kwenye  manyoya na kufika ndani kabisa kwenye ngozi utawaona wakitembeatembea. Wanapenda kukaa kwenye kwapa za kuku na kwenye ngozi ya mwili wake

Usipojua vizuri kuhusu wadudu hawa unaweza ukadhani kuwa kuku wako wanaumwa ugonjwa mwingine kabisa katika magonjwa ya kuku. Na kwamba utahangaika kutumia gharama nyingi za madawa huku kuku wako wakiendelea kuzorota bila kupata nafuu ya matibabu unayohatumia.

Ni muhimu kabla ya kutibu kuku wako ukawasiliana na mtaalamu wa mifugo (Ofisa Ugani) aliye karibu yako ili aweze kukusaidia kukukagulia na kubaini tatizo halisi la kuku wako.  Kwa maana kuku hawahitaji mchezo wa kubahatisha. Unatakiwa ujue ni tatizo gani hasa linawakabili kuku wako ili waweze kupatiwa tiba ya uhakika.

Sasa nini kifanyike kama banda lako litakuwa limevamiwa na Visumbufu hivyo?

Kuna dawa nyingi za kutumia, unaweza kutumia Dawa za unga za kunyunyiza mfano Akheri powder au Sevin (Dudu) Dust. Dawa hizi utanyunyiza kuku wako wote mmoja baada ya mwengine kwenye manyoya yao na sehemu zile ambazo zimevamiwa na wadudu hao mfano machoni na kwenye mapanga yao na vilevile utapaswa dawa hizo kunyunyiza kwenye maranda au vumbivumbi la ndani ya banda la kuku kwa sababu vumbi ni makazi mazuri ya Viroboto na Utitiri.

Lakini wakati mwingine unaweza kujitahidi kutumia dawa hizo za kunyunyiza kwenye mabanda na kuku wenyewe lakini zisifue dafu. Mara nyingi nimeliona hili  kwenye mabanda mengi ya wafugaji. Sasa ukifikia katika hali hii ufumbuzi wa haraka ni kufanya usafi wa banda lako lote. Ondoa maranda na  vumbi lote la samadi kisha deki kwa kutumia dawa ya V- RID Disinfectant.

Pia utapaswa kupuliza dawa hiyo katika kuta za banda lako. Ukiona tabu kufanya hivyo basi baada ya kuondolewa samadi yote katika banda lako la kuku na kufuta vumbi ukutani, deki kwa maji vizuri bila dawa kisha baada ya banda kukauka vyema paka chokaa kote sakafuni ukutani hadi darini kama banda lako lina dari na kama halina basi utaishia tu katika kuta za banda na sakafuni.

Baada ya kukamilisha zoezi hilo ogesha kuku wako wote kwa kutumia dawa ya Paranex, Tik Tik au dawa yoyote ya kuogeshea mifugoiliyochanganywa kwenye maji yaliyowekwa kwenye dishi kubwa la lita ishirini au arobaini au hata ndoo unaweza kitumia. Uogeshaji utafanyika kwa namna ya kumtumbukiza kuku mmoja mmoja  katika lile dishi au ndoo kisha utamtoa.

Ni tendo linalotumia chini ya nusu dakika. Unamtumbikiza unamtoa unamtumbikiza tena unamtoa ni kama mara mbili hivi lengo ni kuhakikisha kuwa dawa inapenya vizuri katika kila sehemu ya mwili wake.

Baada ya kukamilisha zoezi hilo basi kuku wako watarudi bandani wakiwa wako vizuri na visumbufu vyote vikiwa vimetokomezwa kabisa. Kutokea hapo utaanza kuona sasa afya ya kuku wako ikianza kuimarika na kama walikuwa walishaanza kutaga watarudi katika utagaji wao wa kawaida.

Muhimu
Unapotumia dawa ya kuogesha ni vizuri zoezi hili likafanyika mchana wakati jua linawaka ili kusudi kuku waweze kukingwa na athari ya baridi itakayowasababishia kupata nimonia. Vilevile ni vizuri ukawa na mtaalamu karibu atakayekusaidia kuchanganya dawa kwa uwiano sahihi na maji ili kuepusha madhara kama dawa haitachanganywa katika uwiano.

Nipende kukushukuru kwa kuwa pamoja na sisi kwa kipindi chote na pia kuwa mvumilivu na kuendelea kusoma makala zetu....

Jumamosi, 12 Agosti 2017

Mchanganuo wa chakula cha kuku wa nyama(broiler)

JINSI YA KUTENGENEZA CHAKULA CHA KUKU WA NYAMA (BROILER)

1. Mahindi.                  410kg
2. Mashudu alizeti.        90kg
3. Mashudu ya pamba 120kg
4. Dagaa.                        80kg
5. Damu.                         20kg
6. Polard.                      100kg
7. Pumba ya mahindi.  100kg
8. Chokaa.                      55kg
9. Mifupa.                      19kg
10. Chumvi.                     3kg
11. Premix.                   2.5kg

GROWER MASH

mahindi.                380 kg
pumba.                   230kg
dagaa.                      60kg
mifupa.                     10kg
rice polish.              175kg
mashudu ya alizeti 100kg
chokaa.                     40kg
chumvi.                    2.5kg
premix.                    2.5kg
=                          1000kg

CHICK MASH

mahindi.                 530kg
pumba.                    250kg
mifupa.                     15kg
lysine.                      0.5kg
chumvi.                    2.5kg
chokaa.                    2.5kg
mashudu ya alizeti 197kg
dcp.                         0.5kg
premix.                   2.5kg

Jumamosi, 8 Julai 2017

Tangaza nasi ilikupanua wigo zaidi 
kwa maana ya kuwafikia Wateja wengi. Ni rahisi sisi tutakutafutia wateja, wakipatikana kwa kila bidhaa moja tutachukua 10% ya bei ya kuuzia. Mfano vifaranga unauza 2500@ kwahiyo 10% ni 250. Karibu sana









Alhamisi, 6 Julai 2017

Mambo ya muhimu kuzingatia kabla na wakati wa chanjo

Mambo muhimu ya kuzingatia

Ni muhimu kuzingatia kwa makini masharti ya utengenezaji wa chanjo, hii inamaana kubwa sana katika zoezi zima la chanjo, maana ukikosea masharti hayo husababisha madhara kwa mtumiaji na kuku wake pia. Moja ya vitu vya msingi ni kuhifadhi sehemu iliyoelekezwa kwenye karatasi la maelekezo lililobandikwa kwenye chupa na muuzaji, kutayarisha chombo cha kuwekea dawa na lazima kiwe kisafi na njia inayotumika kumchanja kuku wako, hii ina maana kuna nyingi kama vile kwa kuchanja kwenye maji au kuchoma sindano.

Kufuata ushauri wa daktari wa mifugo unapoandaa program ya chanjo. Kimsingi hizi chanjo mara nyingi huwa zinachanjwa na wataalamu lakini kutokana na changamoto za ufugaji wao, inabidi wafugaji wawajibike wenyewe katika zoezi zima la chanjo japo sio chanjo zote lakini chanjozile za vidonge na maji ni rahisi sana kwa mfugajimwenyewe kuzifanya nyumbani. Suala la kuzingatia ni kufuata ushauri na maelezo utakayopewa, kwa mfano chanjo ya new castle ile ya kidonge maelezo yake, ni muhimu; ihifadhiwe kwenye friji ili isipate joto na ukisha changanya kwenye maji inatakiwa itumike ndani ya masaa mawili tu zaidi ya hapo inahalibika.

Chagua aina ya chanjo kulingana na umri na hali ya kiafya ya kuku hapa ni muhimu sana kuzingatia sababu kila chanjo ina mpangilio wake na umri, sio kila chanjoinatumika kwa kila kuku. Zipo chanjo nyingi kama vile mareks, new castle, Gumboro, chanjoya ndui na chanjo ya typhoid. Lakini zote hizi zinatolewa kulingana na umri sio wakati wote zinatolewa. Mfano Mareks ni chanjo ambayo hutolewa mapema pindi kifaranga kimetolewa na kufuatiwa na chanjo ya kideri.

Tumia maji ambayo hayajawekwa dawa kwa ajili ya kuchanganyia chanjo. Maji ni sehemu muhimu sana katika zoezi la chanjo kwa sababu kwa chanjo zile ambazo ni muhimu kuchanganya na maji, suala la msingi la kuzingatia ni maji safi, yasiyo na dawa kwa maana maji ya bomba mara nyingi huwa yanakuwa yame changanywa na dawa, kwa hiyo hayafai. Maji ya kutumika ni ya kisisma, ya muua.

Changanya chanjo ukiwa mbali na kuku kabla ya kuandaa chanjo yako hakikisha kuku wako wamo bandani au mbali na wewe ili kuzuia kuharibu utaratibu mzima wa uandaaji wa chanjo, maana kuku wana tabia ya kufuata kitu hata kama wamekuzoea.

Ni muhimu kupata ushauri kabla wa daktari wa mifugo, kabla ya kuchanja kuku wagonjwa. Kuku mgonjwa hachanjwi, ukimchanja anakufa. Hivyo unafanyaje unapokuwa na kuku mgonjwa ambaye inawezekana ulipo mtoa hakuchanjwa. Pata ushauri wa daktari ambaye atamchunguza kuku wako na kujua anasumbuliwa na nini na nini apewe ili aweze kupona. Wafugaji wengi huwajumlisha kuku wote katika chanjo kitu ambacho ni kosa.

Chanjo zinazochanganywa kwenye maji hutumika ndani ya masaa mawili tu,si zaidi ya hapo. Hiki ni kipengele muhimu kwenye zoezi zima la chanjo, chanjo za aina hii hutumika ndani ya masaa mawili tu ikizidi inakuwa sumu ambapo unaweza zalisha tatizo jingine kama vile kuku kufa ghafla na ili kuweza kufanikisha zoezi hili wapatie pumba kwa wingi kuku wako ambayo itawafanya wapate kiu kabla ujawapa chanjo ili baada ya kupata kiu ukiwapa chanjo watakunywa yote ndani ya muda mfupi.

Kumbuka kuweka kumbukumbu za uchanganyaji vizuri . hapa wafugaji wengi imekuwa imekuwa changamoto sana. Lakini ni moja ya sehemu muhimu za zoazi la chanjo ili kuwa kinga kuku wako, ni muhimu sababu kuna baadhi ya chanjo ambazo zinarudiwa baada ya muda Fulani. Mfano chanjo ya new castle hii kuku akishafikisha miezi mitatu kwa maana wakifikisha miezi sita watapewa tena, hata Gumboro n.k 

Hitimisho, ukizingatia haya chanjo yako itakuwa imefanyika salama na kuku wako kuwa na afya njema na hata siku moja huwezi kuwa na wasiwasi wa magonjwa kama vile ndui, kideri n.k.Kumbuka hutakiwi kufanya mambo yafuatayo unapochanja kama vile; chanjo iliyopita muda wake,kuku ambao wamepitiwa dawa aina ya antibiotiki, kuchanja zaidi ya chanjo moja kwa wakati na kumwaga chanjo ovyo na kuchafua mikono au nguo.

Jumatatu, 22 Mei 2017

Fahamu kwanini Kuku wako anaharisha damu.

KUHARA DAMU ( COCCIDIOSIS)

Protozoa ni vimelea ambayo husababisha ugonjwa huu. Rika zote za kuku hushambulia na ugonjwa huu.

JINSI UNAVYOENEA
Chakula chenye kinyesi au maji yenye ugonjwa huu yanaweza pelekea kuku kuambukizwa.

DALILI
•Kuharisha kinyesi kilichochanganyika na damu
•Kuku kujitenga na wenzie au wengine bandani
•Kupoteza hamu ya kula
•Mabawa kushuka na kuzubaa
•Kudhoofu a kupungua uzito

TIBA
Dawa aina ya AMPROLIUM, OXYTRACYCLINE au SALFA

KINGA
•Usafi wa banda na vyombo vya chakula na maji
•Tenganisha vifaranga na kuku wakubwa
•Ikifika umri wa siku saba vifaranga wapewe AMPROLIUM kwa siku 3, hata kama dalili za ugonjwa hazijajitokeza

Jumapili, 21 Mei 2017

Madhara ya kutojua kuchanganya virutubisho sahihi, yatatokea

MAGONJWA YANAYOWEZA KUSABABISHWA NA UPUNGUFU WA CHAKULA AU VIINI LISHE
Iwapo kuku watapewa chakula chenye viini lishe kidogo au kisicho na viini lishe muhimu kama vile; Protini, wanga, madini na vitamini wanaweza kupata madhara yafuatayo

•Kudumaa
•Kupungua uzito
•Kupungukiwa na damu
•Mifupa kupinda au kuvimba au kutokuwa imara
•Utagaji wake pia huwa hafifu, ganda la yani huwa laini
•Manyoya huwa machache na laini.
•Kuwa na maji mengi mazito chini ya ngozi ya kifuani
•Kupata magonjwa Mara kwa mara

Naman ya kuzuia

Kuku wapewe chakula chenye mchanganyiko wa viini lishe vyote muhimu kama vile vitamini, madini na chokaa kufuatana na umri.

Jumanne, 16 Mei 2017

Je? Kuku wako wanavimba macho.

MAGONJWA SUGU YA MFUMO WA HEWA

Chanzo cha maambukizi

• Maji na chakula kilichochafuliwa na kinyesi cha kuku wagonjwa na kwenye vimelea
• Kupitia mfumo wa hewa kutoka kuku wagonjwa
• Kupitia mayai, hivyo maambukizi huendelea kutoka kizazi hadi kizazi

Dalili

• Kuku kukoroma
• Kuku hutoa makamasi
• Kuku wanakohoa kwa muda mrefu, wiki hadi mwezi
• Kuvimba macho
• Kutingisha kichwa
• Vivo vya kuku viaweza kufikia hadi asilimia 20
Uchunguzi

Kamasi nzito zenye usaha zilizotapakaa kwenye pia, koromeo, mapafu na vifuko vya hewa

Tiba
Madawa aina ya sulfa na antibiotiki



 

mail

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner