KUKUKIBIASHARA: Kuku
Breaking News
Loading...

Ad

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kuku. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kuku. Onyesha machapisho yote

Jumamosi, 10 Februari 2018

Hii ni mifumo ambayo inatumika kufugia kuku Tanzania

Aina za ufugaji wa kuku
Kuna aina mbili za ufugaji wa kuku katika nchi ya Tanzania

1. UFUGAJI URIA

kuku wanajitafutia chakula wenyewe. Aina hii kuku hufungiwa bandani usiku lakini mchana hufunguliwa na kuachwa wajitafutia chakula na maji wenyewe kasha hurudi tena bandani usiku. Na ndio mfumo ambao kaya nyingi za kitamzania zinautumia.

Faida ya ufugaji uria

i. Hakuna gharama za chakula
ii. Kuku hujipatia aina mbali mbali za vyakula kama wadudu, majani na nafaka hivyo hujipatia mlo kamili.
iii. Mtaji, wake ni mdogo kwani hutumia ujenzi rahisi wa mabanda.
iv. Kuku wanaofungiwa kwa njia hii huwa na chanjo.
v. Kuku hawavunji mayai hawapigani, wala kunyonyoana manyoya.

Changamoto

i. Ni ngumu kuzuia minyoo na magonjwa.
ii. Kuku wadogo (vifaranga) huliwa na wanyama na ndege. Mayai hupotea na kuliwa na viumbe waharibifu.
iii. Kuku hupata shida ya mvua na baridi.
iv. Kuku wanaofungiwa kwa njia hii huwa na chanjo.
v. Nafasi kubwa huitajika kwa ajili ya kuwapa kuku nafasi ya kujitafutia chakula cha kutosha.

2. UFUGAJI NUSU URIA

Aina hii ya kuku hujengewa banda na uzungushiwa senyenge kuzuia kuku wasifike mbali na chakula na pia hujengewa sehemu ya kutaga mayai.

Faida

I. Ujenzi ni rahisi
ii. Mbolea usambaa kwa urahisi shambani
iii. Ni rahisi kuzuia na kukinga magonjwa.
iv. Ni rahisi kuokota mayai na pia mayai hayo hayaliwi na wanyama wasumbufu.
v. Hupungua gharama za chakula kwani kuku ujotafutia na kupewa kiasi kidogo cha nyongeza.

Kuna aina mbili za kufuga kuku wa ndani

i) battery cage system.
ii) deap litre system.

Tanzania hutumia njia deap litre system ambapo maranda ya mbao, majani ya mpunga, ngano na pumba za mchele hutumika sakafani kiasi cha 10-15 za ujazo.
- tandiko ambalo ubadilishwa mara tu linapobonyea au kuchanganyika na mbolea au kila baada ya miezi mitatu (3)
- kuku hupewa chakula, kuwekewa viota vya kutagia kuku afugwe kwa kufuata vipimo vya eneo ambavyo ni kuku 2-3 kwa 1m2
- banda hujengwa urefu wa 60 cm kwa tofali au udongo sehemu inayobaki huwa ni kwa kuruhusu mzunguko wa hewa.

Faida zake

1. Kuku wengi hufugwa katika sehemu ndogo
2. Kuku hupata kinga za hali ya hewa, mvua, jua na baridi. Pia hukingwa zaidi na wanyama wasumbufu kama mwewe, panya na nyoka.
3. Mayai hukusanywa kwa urahisi.
4. Kuku hufugwa kibiashara rahisi kukinga magonjwa na wadudu.
5. Mbolea hupatikana kwa wingi.

Changamoto

1. Chakula kisipochanganywa vizuri hakitumiki
2. Gharama kubwa hutumika kujengea banda.

Hizi ni aina za kuku wanaopatikana Tanzania

AINA ZA KUKU
kuna aina kuu mbili za kuku
1. Kuku wa asili ( kuku wa kienyeji)
2. Kuku wa kisasa

Kuku wa asili
Hawa utofautiana katika maumbo, utagaji, uzito, rangi ya manyoya, ukuaji na uwezo wa kutaga mayai. Kuku wa kienyeji hukua taratibu na utaga mayai machache.

Kuku wa kisasa (zaotic breed)
Hawa ni kuku toka nchi za kigeni pia wana aina mbili ambazo ni
i. Kuku chotara
ii. Pure breed

Kuku chotara
Ni mchanganyiko wa aina mbili au zaidi ya kuku. Siku hizi kuku wanaotakiwa kibiashara ni kuku chotara ( wengine ni wa mayai na wa nyama)

Pure breed
Hawa wanagawanyika sehemu mbili kuku (a) kuku wazito ( hutoa nyama) broiler
(b) kuku wepesi ( hutaga mayai) layers

Jumapili, 3 Desemba 2017

MAMBO SITA (6) YA KUHAKIKISHA UZAO WA KUKU WAKO

Karibu sana ndugu msomaji na mfuatiliaji wa makala hizi za ufugaji wa kuku aina zote kulingana na fursa tuliyonayo katika nchi yetu. Nimatumai ya kwamba u mzima wa afya
Karibu katika mada ya leo ambayo itakusaidia kuweza kutatua changamoto ya kuweza kuwa na kuku wengi kwa kadri, Mungu atavyo kujalia uhai.
Mada yetu ya leo inahusu izao wa uhakika wa kuku wako bila kubahatisha. Hasa kwa wafugaji wa kuku wa kienyeji majumbani kwetu. Tumekuwa na mazoea ya kumwachia kuku ajilee mwenyewe na kutarajia kupata kitu bora. Katika uharisia haiwezekanai. Ufwatiliaji wa karibu ni muhimu ili kujihakikishia angalai asilimia 80 hadi 90 ya kufanikisha kile unachokitaka.
Yafuatayo ni mambo sita (6) ya kuhakikisha uzao wa kuku wako
1. Kuchukua mayai kila yanapotagwa.
Kuku pindi atakapofikia kuanza kutaga mayai, ni muda muafaka kuanza zoezi hili la hatua ya kwanza lakini subiri atakapo taga mayai mawili hadi matatu ndipo uanze kuchukua na hapo naomba tuelewane kwamba, kuku wako akifikisha mayai mawili itakuwa na maana ni siku yake ya pili kutaga. Kuku kwa kawaida hasa wa kienyeji hutaga yai moja kwa siku. Hivyo zoezi la kuchukua mayai ni pale atakapotaga yai la tatu ndipo uchukue na kuacha yale mawili yaliyotangulia kutagwa. Ni muhimu sana kuchukua yai jipya.
2. Kuweka alama katika kila yai .
uwekaji wa alama katika mayai ni muhimu sana ili kuweza kutambua yai limetagwa lini na kwa pendekezo hakikisha una kalamu ya mkaa (penseli) na uweke alama ya namba ( kama vile 1, 2, 3,.......) hii itasaidia kujua ni yai la ngapi kutagwa tangu kuku wako aanze kutaga. Kabla ya kuweka alama hakikisha mikono yako haina harufu yoyote ile, hivyo kama mikono yako ina harufu, chukua majivu yanawe kama maji, yatakusaidia kuondoa harufu. Andika namba kwenye yai moja kila linapotagwa kwa kuanza na namba moja na kuendelea.
3. Kuhifadhi sehemu salama.
Baadaya kuchukua na kuweka alama hakikisha umeanda sehemu nzuri ambayo haina joto na watoto hawawezi kuchezea. Sehemu hiyo inaweza kuwa kwenye treyi lako au boxi ambalo umeweka malanda ya mbao au pumba ya mpunga na kuyapanga vizuri kulingana na namba ulizo weka kama alama na kimsingi utakuwa umeanza na yai la tatu tangu kutagwa. Hakikisha sehemu uliyoweka hakuna joto maana yai likipata joto litaharibika.
4. Kuchuka mayai yasiyozidi wiki mbili kwa ajili ya kuatamiwa.
Yai bora kwa ajili ya kuatamiwa ni lile lisilozidi wiki mbili tangu kutagwa. Katika zoezi hili hakikisha unachukua mayai yote uliyoyahifadhi. Kuku aliye vizuri katika utagaji hutaga mayai kumi na tano hadi ishirini, hivyo kwa kuwa uliweka alama katika mayai uliyo ya hifadhi anzia namba ya mwisho kuandikwa kurudi nyuma,kwa maana anza na yai la mwisho kutagwa kurudi nyuma lakini hakikisha unakumbukumbu ya tarehe ya kuku alipoanza kutaga, hiyo itakusaidia kujua mayai ya wiki mbili tangu kutagwa ni yapi. Muwekee kuku mayai 12 hadi 15 kulingana na umbo la kuku wako. Mfano kuku wako kataga mayai 15, hivyo utachukua yai la 15 hadi namba ya yai itakalo kuwa ndani ya muda unaofaa. Kuku wa kienyeji hutagi siku zote mfululizo kuna baadhi ya siku anaruka kwa hiyo hayo mayai kumi na tano yanaweza kuwa yametagwa kwa wiki tatu.
5. Siku ya kumi baada ya kuatamiwa, yapime mayai.
Hii ni sehemu au zoezi muhimu sana ilikuweza kujua kuwa mayai yaliyoatamiwa yatafaa au la. Upimaji hufanyika usiku kwa maana giza likiingia ambapo kuku wote watakuwa bandani. Zoezi hili linaitaji watu wawili ili kuweza kufanikisha. Mmoja kumshika kuku na mwingine kufanya zoezi la upimaji.Chukua tochi, mikono ya mpimaji isiwe na harufu, hivyo kujiridhisha kwa kunawa majivu na kuanza zoezi la upimaji. Chukua yai mojamoja, halafu kiganja chako kimoja kitengeneze umbo la sifuri kwa kutumia kidole gumba na kidole kinachofuatia baada ya hapo weka yai kwa juu yake kwa kutanguliza sehemu iliyochongoka iwe chini. Halafu chukua tochi na murika kwa chini kule kulikochongoka yai, utaona mambo mawili kwanza, kama yai ni zima utaona kitu cheusi ndani ya yai ujue linafaa kuendelea kuatamiwa. Pili, kama utaona yai ni jeupe ( transparent) ujue ilo yai halifai kwa kutotolewa. Zoezi litaendelea mpaka mayai yote yaishe hapo utakuwa umejihakikishia kuwa ni mayai mangapi mazima na yatatotolewa.
6.kutotolewa kwa mayai yote yaliyoatamiwa
Mpaka kufika hapo zoezi zima litakuwa limefanikiwa kwa asilimia 90 hadi 100 kwa maana ya kutotolewa vifaranga vyote ambavyo katika upimaji utakuwa umejiridhisha kuwa ni mayai mangapi yatatotolewa na ni uhakika idadi iyo iyo ya upimaji kufika katika utotolewaji.
Hitimisho, nipende kusisitiza kuwa katika zoezi zima la hatua ya kwanza hadi ya mwisho mayai yako yawe yamewekwa kwa kutanguliza sehemu iliyochongoka chini na pana juu hasa kwenye hatua ya kuhifadhi pindi unapoyachukua yanapotagwa. Nikushukuru ndugu msomaji kwa kuwa nami tangu hatua ya kwanza hadi ya mwisho. Hakiki utakuwa umepata kitu na kukifanyia kazi. Karibu sana tena katika makala zinazofuata

Jumapili, 26 Novemba 2017

Vifaranga wa kienyeji kabisa

https://youtu.be/k-BYOqoLCoY

Ijumaa, 28 Aprili 2017

ULEAJI BORA WA VIFARANGA

Kuna vitu vya msingi katika uleaji wa vifaranga vya kuku. Uleaji huu hutofautiana kati ya vifaranga wa kuku wa mayai, kienyeji na kuku wa nyama katika chakula na chanjo kwa ujumla
MATAYARISHO
* Banda liwe imara kuepuka wizi na wanyama wasumbufu kama ngoja, paka, mbwa, mwewe, na kecheche.
* Banda liwe linaweza kuingiza hewa ya kutosha na kavu isiyo na unyevunyevu.
*kabla ya kuingiza safisha banda nje na ndani kwa kutumia dawa ya kuua vijidudu vya magonjwa. Paka chokaa kuta za ndani na hakikisha banda haliwi na joto Kali, baridi kuingiza, mbua na upepo mkali.
*Tayarisha chakula bora.
* vifaa vya kulishia na kunyweshea maji.
* tandiko safi, kama vile maranda, pumba za mchele.
*Dawa
KABLA YA KUFIKA VIFARANGA
Banda liwe tupiu kwa wiki moja baada ya kusafisha kwa dawa. Vifaranga utakaopewa watoke kwenye mzalisha mwenye historian nzuri.
* usichanganye vifaranga wa sehemu tofauti.
* vifaranga huweza kuathirika haraka na mazingira hivyo yafaa kuwa na uangalifu wa hewa, mwanga na joto.
* vifaa vya mwanga na joto ni muhimu na lazima katika kulea vifaranga.
* tangazi za msuara kwa kutumia hard board yenye urefu wa sentimita 60 na katikati weka balbu au Niko la mkaa na taa ya mafuta; Kwisha mwanga wa kutosha ili vifaranga waone chakula na maji.
* weka chokaa halafu maranda na tandiko chilk paper au magazeti juu.   ya maranda.
* Masaa matano kabla ya kufika vifaranga washa taa za joto au jiko la mkaa kwa ajili ya joto kwa vifaranga, joto liwe na nyuzi joto 32-35.
* Hakikisha joto loinakuwa la wastani.
    Wiki ya kwanza - 35°c
    Wiki ya pili         - 32°c
    Wiki ya tatu       - 29°c
    Wiki ya nne        - 26°c
MUHIMU
Iwapo vifaranga wanatoka mbali na wamechoka wape glucose au sukaei kidogo kwenye maji ( kijiko cha chakula kwa kila Lita tank za maji).
KUPOKEA VIFARANGA
Watoe vifaranga kwenye maboksi kwa haraka na kuwaingiza kwenye mduara au hard board uliyoiandaa na hakikisha unayo hesabi kamili.
* vifaranga wore kwenye maji ya glucose watoe nauwanyweshe wale wore ambao hawakunywa maji.
* Baada ya masaa mawili weka chakula kwenye vyombo hakikisha kuna mwanga saa 24 na joto la kutosha.
 


Enter your email address:


Delivered by FeedBurner

Jumatano, 26 Aprili 2017

Fuga kuku mwenye faida

KUROILER

Wafugaji wengi wa kuku wametamani sana kufuga mbegu bora ya kuku hasa wa kienyeji ili kupata matokeo mazuri katika biashara, hasa pale tunapozungumzia uuzaji wa kuku unategemea sana uzito wake,  ambapo mbegu ya kuku wa kienyeji kwa mtetea ni uzito wa kilo 1.8 wastani na jogoo ni kilo 2.5, ambao ni uzito Mdogo sana labda kwa jogoo kidogo sio mbaya lakini kwa mtetea ni Mdogo sana kupeleka sokoni.Changamoto hii imepelekea wafugaji wengi kupoteza masoko na wengine kukosa kabisa. Hivyo basi kumepatikana sululisho la changamoto, maana kwa Tanzania sasa imepatikana mbegu bora kabisa inayokata kiu ya wafugaji wengi ambayo inaitwa KUROILER. Kuku huu ni mbegu chotara mwenye Sifa sawa na kuku wa kienyeji. Sifa zake ni kama zifuatazo

Wana rangi kundi
Kuku hawa wanavutia sana kwa kuwa tazama, kutoka na rangi zao nzuri. Wengi wake wanarangi ya kanga Yaani madoadoa. Pia sio hiyo tu wanarangi nyingine ambazo ukiwafuga wanavutia sana kuwatazama. 

Chakula
Ulaji wa kuku huyu ni wa kawaida kama alivyo kuku wa kienyeji. Kwa maana ya kwamba anaweza jitafutia mwenyewe kwa kuachwa nne na kuokota wadudu mbalimbali pamoja na mabaki tofauti tofauti, pia kama utakuwa na utaratibu wa kununua chakula cha dukani anakula bila shida yoyote, kutengeneza mwenyewe kwa kununua mahitaji mbalimbali ambayo ni muhimu kwa chakula, mfano chakula vya protini, wanga, madini na chumivi. Vyovyote takavyo taka apate chakula chake anakula bila tabu. Bila kusahau pia unaweza mpa mabaki ya chakula nayo yanafaa.

Anafugwa kienyeji

Kuku huyu hutaga mayai lakini halalii, hivyo inambidi mfugaji achukue jukumu la kumlea kifaranga kama ambavyo mtetea angemlea. Hii inamaanisha kuwa kifaranga ataitaji joto cha chakula ili akue na baada ya miezi, utamwacha ajitafutie chakula mwenyewe kama ilivyo kwa kuku wa kienyeji. Anauwezo wa kutafuta chakula kwa kula wadudu, mabaki na vitu vingine ambayo vinafaa kuliwa

Utagaji wao

Kuku hawa wanauwezo wa kutaga kwa muda wa  miaka 3 na hawalalii mayai yao.Mayai yao huwa na mbegu kwa maana ya kwamba, yai lenye mbegu maana yake kuku ametaga yai hilo kwa kupandwa na jogoo. Kumbuka kuku aina yoyote anauwezo wa kutaga yai bila kupandwa na jogoo na kutaga lakini yai hilo halitakuwa na mbegu ndani yake kama ilivyo kwa kuku wa kisasa wa mayai. Kwa maneno mengi yai yenye mbegu likilaliwa nitatoa kifaranga. Kingine yani la kuku huyu hufaa kuanguliwa. Pia idadi ya mayai ni 200 hadi 250 kwa mwaka.

Uzito wako

Kuku hawa wanauzito mkubwa ukilinganisha na kuku wa kawaida au kienyeji.Maana mtetea anaanzia kilo2 hadi 3 na jogoo anaanzia kilo 3 mpaka kilo5. Kwanza wanasifika kwa kuwa na nyama nyingi na watamu pia lakini sio kwamba kwa kilo hizi kuna maanisha hawa kui kwa muda sahihi lahasha kilo hizo ni kuanzia miezi mitano na kuendela.

Mayai yao 

Mayai yao huwa na rangi huwa tofauti na kiini chake huwa cha njano.Na ili kupata kiini cha njano kama ilivyo kwa kuku wengine kuroiler anatakiwa ale majani. Kingine mayai yake ni makubwa kuliko ya kuku wa kienyeji na mara nyingi hutotolewa na machine ya kutotoleshea vifaranga.

Huhimili
Kuku huyu anahimili sana magonjwa kama ilivyo kwa kuku wa kienyeji. Cha muhimu ni kuzingatia chanjo kama zinavyoitajika, hii itakusaidia kuwakinga na magonjwa kama kideri na mengine

hitimisho

Baada ya kupata Sifa hizi za kuku aina ya kuroiler, chukua maamuzi sasa kwa kufuga mbegu bora na yenye faida kwa mfugaji tofauti na mbegu ya kienyeji kabisa ambayo haina mchanganyiko wowote. Ushauri nilikuwa na ufugaji mwenye faida ni kuwekeza nguvu, ajili na pesa katika Kuku ndipo utapata faida lakini vinginevyo tutaishia kuona fursa hii haina maslahi yoyote.

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

Jumamosi, 22 Aprili 2017

Fahamu aina mbalimbali za kuku wa kienyeji

KABILA ZA KUKU WA KIENYEJI
Kuna makabila tofauti ya kuku wa kienyeji, ni ngumu kidogo kuweza kuyachanganua makabila hayo kutokana na muingiliano mkubwa wa vizazi kati ya aina mbalimbali za kuku hao. Hata hivyo kuku hawa wana tofauti za kimaumbile zinazosaidia kwa kiasi fulani kutambua uwepo wa baadhi ya makabila ya kuku. Kabila hizi pia zinahusishwa kwa kiasi kikubwa na eneo kuku wanakotoka. Baadhi ya kuku wa kienyeji wanaweza kutambuliwa kwa maumbile yao Mfano:

a. Kishingo - kuku wasio na manyoya shingoni

b. Njachama au Nungunungu - Hawa ni wale wenye manyoya                           yaliyosimama.

c. Kibwenzi - Ni wale wenye manyoya mengi kichwani.

d. Kibutu- Hawa hawana manyoya mkiani

Mwingiliano wa vizazi unaweza ukasababisha kuku kuwa na aina ya maumbile mchanganyiko. Mfano kuku aina ya kuchi anaweza kuwa na alama ya kishingo, Njachama, Kibwenzi au Kibutu.
Hivyo kabila za kuku zifuatazo zinaweza kutambuliwa kama ndiyo kabila za kuku wa kienyeji kulingana na maumbile yao na maeneo wanakotoka.

KUCHI
Ni kuku warefu kwa umbo na wenye kusimama mgongo ukiwa wima. Wana manyoya machache mwilinini na hasa kifuani, vilemba vyao ni vidogo. Majogoo huwa na wastani wa uzito wa Kg. 2.5 na mitetea kg 1.5 mayai ya kuchi yana uzito wa wastani wa gm 45. Kuku hawa hupatikana kwa wingi maeneo ya Mwanza, Shinyanga, Tabora na Zanzibar.

CHING'WEKWE
Kuku hawa ambao jina lao ni gumu kidogo kwa mtu asiyekuwa na meno kulitamka wana sifa zifuatazo.
Majogoo wana wastani wa kg 1.6, Mitetea wastani kg 1.2, mayai wastani wa gm 37. Kuku hawa wenye umbo dogo hupatikana zaidi maeneo ya CHAKWALE mkoani Morogoro na pia sehemu za umasaini. Kuku hawa hutaga mayai mengi sana kuliko aina nyingine ya kuku wa kienyeji waliopo Tanzania, kwa hiyo wanafaa sana kwa biashara ya mayai.

UMBO LA KATI
Majogoo wana uzito wa wastani wa kg. 1.9, Mitetea kg. 1.1, Kuku hawa ndio hasa wanaoitwa wa kienyeji(wa kawaida) Wana rangi tofauti. Utafiti umeonyesha kuwa kuku hawa hukua upesi na hupata kinga upesi baada ya kuwachanja dhidi ya ugonjwa wa mdondo (Castle desease)
Muhimu - Mfugaji akifanya uchaguzi kutoka kwenye aina hii ya kuku na kutoa matunzo mazuri kwa hao kuku waliochaguliwa, Hakika anaweza kupata kuku walio bora na wenye uzito wa kutosha pia kutaga mayai mengi na makubwa.

SINGAMAGAZI
Ni aina ya kuku wakubwa wa kienyeji wanaopatikana zaidi TABORA, kuku hawa wana utambulisho maalum kutokana na rangi zao. Majogoo huwa na rangi ya moto na mitetea huwa na rangi ya nyuki. Uzito - Majogoo uzito wa wastani wa kg 2.9, mitetea wastani wa kilo 2 mayai gramu 56.

MBEYA
Kuku hawa wanapatikana Ileje mkoani mbeya. Asili hasa ya kuku hawa ni kutoka nchi ya jirani ya Malawi na si wa kienyeji asilia bali wana damu ya kuku wa Kizungu "Black Australop". Majogoo Kg 3 mitetea kg 2 mayai gram 49

PEMBA
Hupatikana zaidi Pemba. Majogoo Kg.1.5 Mitetea Kg 1 mayai wastani gm 42

UNGUJA.
Majogoo Kg 1.6,mitetea kg 1.2 mayai gm 42. Kuku hawa wa Unguja na Pemba wanashabihiana sana na Kuchi isipokuwa hawa ni wadogo.

Ijumaa, 21 Aprili 2017

KUKU WA KIENYEJI

AINA ZA KUKU

kuna aina kuu mbili za kuku

1. Kuku wa asili ( kuku wa kienyeji)

2. Kuku wa kisasa


Kuku wa asili

Hawa utofautiana katika maumbo, utagaji, uzito, rangi ya manyoya, ukuaji na uwezo wa kutaga mayai. Kuku wa kienyeji hukua taratibu na utaga mayai machache.


Kuku wa kisasa (zaotic breed)

Hawa ni kuku toka nchi za kigeni pia wana aina mbili ambazo ni

i. Kuku chotara

ii. Pure breed


Kuku chotara

Ni mchanganyiko wa aina mbili au zaidi ya kuku. Siku hizi kuku wanaotakiwa kibiashara ni kuku chotara ( wengine ni wa mayai na wa nyama)

Muhimu

kuku wa kienyeji ni wazuri sana kwa kufuga kibiashara lakini matokeo mazuri ya kuku huyu ni pale atakapofugwa kisasa, hii inamaana kwamba inaitajika chakula kizuri chenye mchanganyiko uliokamilika, banda zuri lenye nafasi,chanjo mbalimbali muhimu kwa ukuaji,uangalizi wa karibu,kutunza kumbukumbu na kuchagua aina nzuri au kabila zuri la kufuga.


 

mail

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner