Mambo muhimu ya kuzingatia
Ni muhimu kuzingatia kwa makini masharti ya utengenezaji wa chanjo, hii inamaana kubwa sana katika zoezi zima la chanjo, maana ukikosea masharti hayo husababisha madhara kwa mtumiaji na kuku wake pia. Moja ya vitu vya msingi ni kuhifadhi sehemu iliyoelekezwa kwenye karatasi la maelekezo lililobandikwa kwenye chupa na muuzaji, kutayarisha chombo cha kuwekea dawa na lazima kiwe kisafi na njia inayotumika kumchanja kuku wako, hii ina maana kuna nyingi kama vile kwa kuchanja kwenye maji au kuchoma sindano.
Kufuata ushauri wa daktari wa mifugo unapoandaa program ya chanjo. Kimsingi hizi chanjo mara nyingi huwa zinachanjwa na wataalamu lakini kutokana na changamoto za ufugaji wao, inabidi wafugaji wawajibike wenyewe katika zoezi zima la chanjo japo sio chanjo zote lakini chanjozile za vidonge na maji ni rahisi sana kwa mfugajimwenyewe kuzifanya nyumbani. Suala la kuzingatia ni kufuata ushauri na maelezo utakayopewa, kwa mfano chanjo ya new castle ile ya kidonge maelezo yake, ni muhimu; ihifadhiwe kwenye friji ili isipate joto na ukisha changanya kwenye maji inatakiwa itumike ndani ya masaa mawili tu zaidi ya hapo inahalibika.
Chagua aina ya chanjo kulingana na umri na hali ya kiafya ya kuku hapa ni muhimu sana kuzingatia sababu kila chanjo ina mpangilio wake na umri, sio kila chanjoinatumika kwa kila kuku. Zipo chanjo nyingi kama vile mareks, new castle, Gumboro, chanjoya ndui na chanjo ya typhoid. Lakini zote hizi zinatolewa kulingana na umri sio wakati wote zinatolewa. Mfano Mareks ni chanjo ambayo hutolewa mapema pindi kifaranga kimetolewa na kufuatiwa na chanjo ya kideri.
Tumia maji ambayo hayajawekwa dawa kwa ajili ya kuchanganyia chanjo. Maji ni sehemu muhimu sana katika zoezi la chanjo kwa sababu kwa chanjo zile ambazo ni muhimu kuchanganya na maji, suala la msingi la kuzingatia ni maji safi, yasiyo na dawa kwa maana maji ya bomba mara nyingi huwa yanakuwa yame changanywa na dawa, kwa hiyo hayafai. Maji ya kutumika ni ya kisisma, ya muua.
Changanya chanjo ukiwa mbali na kuku kabla ya kuandaa chanjo yako hakikisha kuku wako wamo bandani au mbali na wewe ili kuzuia kuharibu utaratibu mzima wa uandaaji wa chanjo, maana kuku wana tabia ya kufuata kitu hata kama wamekuzoea.
Ni muhimu kupata ushauri kabla wa daktari wa mifugo, kabla ya kuchanja kuku wagonjwa. Kuku mgonjwa hachanjwi, ukimchanja anakufa. Hivyo unafanyaje unapokuwa na kuku mgonjwa ambaye inawezekana ulipo mtoa hakuchanjwa. Pata ushauri wa daktari ambaye atamchunguza kuku wako na kujua anasumbuliwa na nini na nini apewe ili aweze kupona. Wafugaji wengi huwajumlisha kuku wote katika chanjo kitu ambacho ni kosa.
Chanjo zinazochanganywa kwenye maji hutumika ndani ya masaa mawili tu,si zaidi ya hapo. Hiki ni kipengele muhimu kwenye zoezi zima la chanjo, chanjo za aina hii hutumika ndani ya masaa mawili tu ikizidi inakuwa sumu ambapo unaweza zalisha tatizo jingine kama vile kuku kufa ghafla na ili kuweza kufanikisha zoezi hili wapatie pumba kwa wingi kuku wako ambayo itawafanya wapate kiu kabla ujawapa chanjo ili baada ya kupata kiu ukiwapa chanjo watakunywa yote ndani ya muda mfupi.
Kumbuka kuweka kumbukumbu za uchanganyaji vizuri . hapa wafugaji wengi imekuwa imekuwa changamoto sana. Lakini ni moja ya sehemu muhimu za zoazi la chanjo ili kuwa kinga kuku wako, ni muhimu sababu kuna baadhi ya chanjo ambazo zinarudiwa baada ya muda Fulani. Mfano chanjo ya new castle hii kuku akishafikisha miezi mitatu kwa maana wakifikisha miezi sita watapewa tena, hata Gumboro n.k
Hitimisho, ukizingatia haya chanjo yako itakuwa imefanyika salama na kuku wako kuwa na afya njema na hata siku moja huwezi kuwa na wasiwasi wa magonjwa kama vile ndui, kideri n.k.Kumbuka hutakiwi kufanya mambo yafuatayo unapochanja kama vile; chanjo iliyopita muda wake,kuku ambao wamepitiwa dawa aina ya antibiotiki, kuchanja zaidi ya chanjo moja kwa wakati na kumwaga chanjo ovyo na kuchafua mikono au nguo.
0 comments:
POST A COMMENT