Ugonjwa huu ni hatari sana kwa kuku lakini unaweza udhibiti | KUKUKIBIASHARA
Breaking News
Loading...

Ad

Alhamisi, 4 Mei 2017

Ugonjwa huu ni hatari sana kwa kuku lakini unaweza udhibiti

KIDERI
Ni ugonjwa unaosababishwa na virusi ambao hushambulia aina zote za spishi za ndege, ijapokuwa kuku ndio aina inayoathirika zaidi
DALILI
•Vifo vya ghafla bila kuonesha dallili zote
•Kuvimba kwa kichwa na shingo
•Kuhalisha uharo wa kijani
•Utagaji wa mayai kushuka kwa kiasi kikubwa au kusimama kabisa
•Kutetemeka, kichwa kugeuzwa upande mmoja
•Kupooza kwa mabawa na miguu.
JINSI UNAVYOENEA
•Chanzo cha maambukizi ni maji, chakula kill Hoxha fulls a na kinyesi cha kuku wagonjwa.
•Pia maambukizi huweza kupitia mfumo wa hewa ktoka kwa kuku wagonjwa
•Kuku, vifaa vya kazi na bidhaa zitokanazo na kuku ( nyama, mayai, manyoya na mbolea) kutoka mashamba yenye ugonjwa zinaweza kueneza ugonjwa
•Faranga anaweza kupata maambukizi kutoka vituo vya kutotolea vifaranga kutokana na maganda ya mayai yaliyochafuliwa
•Kuku kuzubaa na kuacha kula
•Uku kukohoa, hupiga chafya na kupumia kwa shida
MATOKEO KWA KUCHUNGUZA MZOGA ALIYEATHIRIKA
Ugonjwa huathiri zaidi mfumo wa hewa na njia ya chakula, hivyo mabadiliko yanayoonekana kwenye mzoga ni pamoja
•Madoa a damu kwenye mfumo wa hewa
•Kamasi nzito zenye Tangu ya njano kwenye koromeo
•Utandu mweupe kwenye mfumo wa hewa
•Bandama kuvimba
•Uvimbe kwenye kichwa na eneo la shingo
•Madoa madogo madogo ya damu kwenye kifua, mafuta na utandu wa tumboni
•Damu kuvia kwenye mfumo wa usagaji chakula, juju, firigisi, tumbo na utumbo.
KUMBUKA:
Haya matokeo yatakusaidia wakati pale kuku amekufa banda bila kujua nini tatizo, kabla ya kumtupa mchinje na kumkagua tatizo lilikuwa nini.
KUTHIBITI
Kuna namana za kuchanja kuku wako dhidi ya ugonjwa wa kideri
I.Kudondoshea tone moja jichoni
II.Kwa kidonge
KUDONDOSHEA TONE MOJA JICHONI
•Pata chanjo kutoka kwa wakala au duka la mifugo lililokaribu nawe. Chanjo inayopendekezwa ni chanjo ya kideri 1-2 (1-2 NEWCASTLE VASSINE)
•Kamata kuku kwa uthabiti huku ukiwagemeza upande
•Dondoshea tone moja la chanjo ya kideri kwenye jicho moja
•Subiri kuku achezeshe kope ndipo umuachie.
KWA KIDONGE
•Pata chanjo kutoka wakala au duka la mifugo lililo karibu nawe, hakikisha hifadhiwa kwenye barafu ili isiyeyuke kabla ya kutumika
•Kidonge hicho kimoja kitatumika kwa kuwekwa kwenye kiasi cha maji Lita 20
•Ukisha changanya kidonge na maji, hakikisha inatumika ndani ya Masaa 2 baadaya masaa hayo kupita haitafaa tena kwa matumizi.
MUHIMU:
Chanja kila baada ya miezi 3 kwa kuku umri zaidi ya miezi mitatu na kuendelea  tofauti na vifaranga
Chanja kuku kwenye afya tuu. ( uki chanja mgonjwa atakufa)
KUMBUKA:
Kuku hunyakiyesi cha kijani sio kila kijani ni mdondo HAKUNA TIBA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

google+

linkedin

About Author
  • Naitwa Mordecai Minga,Karibu kwanye blog hii ya ufugaji wa kuku kibiashara zaidi Read More

    Maoni 1 :

     

    mail

    Enter your email address:

    Delivered by FeedBurner