KUROILER
Wafugaji wengi wa kuku wametamani sana kufuga mbegu bora ya kuku hasa wa kienyeji ili kupata matokeo mazuri katika biashara, hasa pale tunapozungumzia uuzaji wa kuku unategemea sana uzito wake, ambapo mbegu ya kuku wa kienyeji kwa mtetea ni uzito wa kilo 1.8 wastani na jogoo ni kilo 2.5, ambao ni uzito Mdogo sana labda kwa jogoo kidogo sio mbaya lakini kwa mtetea ni Mdogo sana kupeleka sokoni.Changamoto hii imepelekea wafugaji wengi kupoteza masoko na wengine kukosa kabisa. Hivyo basi kumepatikana sululisho la changamoto, maana kwa Tanzania sasa imepatikana mbegu bora kabisa inayokata kiu ya wafugaji wengi ambayo inaitwa KUROILER. Kuku huu ni mbegu chotara mwenye Sifa sawa na kuku wa kienyeji. Sifa zake ni kama zifuatazo
Wana rangi kundi
Kuku hawa wanavutia sana kwa kuwa tazama, kutoka na rangi zao nzuri. Wengi wake wanarangi ya kanga Yaani madoadoa. Pia sio hiyo tu wanarangi nyingine ambazo ukiwafuga wanavutia sana kuwatazama.
Chakula
Ulaji wa kuku huyu ni wa kawaida kama alivyo kuku wa kienyeji. Kwa maana ya kwamba anaweza jitafutia mwenyewe kwa kuachwa nne na kuokota wadudu mbalimbali pamoja na mabaki tofauti tofauti, pia kama utakuwa na utaratibu wa kununua chakula cha dukani anakula bila shida yoyote, kutengeneza mwenyewe kwa kununua mahitaji mbalimbali ambayo ni muhimu kwa chakula, mfano chakula vya protini, wanga, madini na chumivi. Vyovyote takavyo taka apate chakula chake anakula bila tabu. Bila kusahau pia unaweza mpa mabaki ya chakula nayo yanafaa.
Anafugwa kienyeji
Kuku huyu hutaga mayai lakini halalii, hivyo inambidi mfugaji achukue jukumu la kumlea kifaranga kama ambavyo mtetea angemlea. Hii inamaanisha kuwa kifaranga ataitaji joto cha chakula ili akue na baada ya miezi, utamwacha ajitafutie chakula mwenyewe kama ilivyo kwa kuku wa kienyeji. Anauwezo wa kutafuta chakula kwa kula wadudu, mabaki na vitu vingine ambayo vinafaa kuliwa
Utagaji wao
Kuku hawa wanauwezo wa kutaga kwa muda wa miaka 3 na hawalalii mayai yao.Mayai yao huwa na mbegu kwa maana ya kwamba, yai lenye mbegu maana yake kuku ametaga yai hilo kwa kupandwa na jogoo. Kumbuka kuku aina yoyote anauwezo wa kutaga yai bila kupandwa na jogoo na kutaga lakini yai hilo halitakuwa na mbegu ndani yake kama ilivyo kwa kuku wa kisasa wa mayai. Kwa maneno mengi yai yenye mbegu likilaliwa nitatoa kifaranga. Kingine yani la kuku huyu hufaa kuanguliwa. Pia idadi ya mayai ni 200 hadi 250 kwa mwaka.
Uzito wako
Kuku hawa wanauzito mkubwa ukilinganisha na kuku wa kawaida au kienyeji.Maana mtetea anaanzia kilo2 hadi 3 na jogoo anaanzia kilo 3 mpaka kilo5. Kwanza wanasifika kwa kuwa na nyama nyingi na watamu pia lakini sio kwamba kwa kilo hizi kuna maanisha hawa kui kwa muda sahihi lahasha kilo hizo ni kuanzia miezi mitano na kuendela.
Mayai yao
Mayai yao huwa na rangi huwa tofauti na kiini chake huwa cha njano.Na ili kupata kiini cha njano kama ilivyo kwa kuku wengine kuroiler anatakiwa ale majani. Kingine mayai yake ni makubwa kuliko ya kuku wa kienyeji na mara nyingi hutotolewa na machine ya kutotoleshea vifaranga.
Huhimili
Kuku huyu anahimili sana magonjwa kama ilivyo kwa kuku wa kienyeji. Cha muhimu ni kuzingatia chanjo kama zinavyoitajika, hii itakusaidia kuwakinga na magonjwa kama kideri na mengine
hitimisho
Baada ya kupata Sifa hizi za kuku aina ya kuroiler, chukua maamuzi sasa kwa kufuga mbegu bora na yenye faida kwa mfugaji tofauti na mbegu ya kienyeji kabisa ambayo haina mchanganyiko wowote. Ushauri nilikuwa na ufugaji mwenye faida ni kuwekeza nguvu, ajili na pesa katika Kuku ndipo utapata faida lakini vinginevyo tutaishia kuona fursa hii haina maslahi yoyote.
0 comments:
POST A COMMENT