KUKUKIBIASHARA
Breaking News
Loading...

Ad

Latest Post

Jumanne, 4 Septemba 2018

USINUNUE KUKU WA KUFUGA KWENYE VYANZO HIVI.


Habari, ndugu msomaji Na mfuatiliaji wa makala zetu za UFUGAJI wa Kuku. Ni matumai yetu u mzima wa afya njema Na ukotayari kutimiza majukumu yako ya kila siku. Pia tuwao.bee wenzetu walio tangulia mbele za haki Amani mana hata sisi tuko njiani kuelekea huko.
Tulejee kwenye somo letu la Leo kama linavyojieleza hapo huu. Mdau yoyote anapotaka kuanza kufuga Kuku Mara nyingi huwa anajiuliza atapata wapi Kuku hapo wa kufuga Na pia kuna sehemu nyingi sana ambazo unaweza kupata Kuku wa kufuga lakini sehemu au vyanzo hivi usinunue Kuku wako wa kufuga, navyo ni..
Sokoni ni sehemu mojawapo ambayo Kuku huuzwa kwa ajili ya watu wanaotafuta ili wasiangaike kwenda vijijini au kwa mana nyingine sokoni ni sehemu ambayo inarahisisha upatikanaji wa bidhaa kama Kuku. Sasa kwa mtu ambaye anataka kufuga Kuku kama mradi, sokoni siyo sehemu sahihi kwa sababu Mara nyingi Kuku wale huwa wanatolewa kwenye vyanzo visivyofuata taratibu za ufugaji, kwa mana unaweza nunua Kuku wako pale Na baada ya siku chache wanaanza kuugua Na kufa. Mara nyingi Kuku wale hawana chanjo Na wengine wanakuwa wagonjwa. Hivyo wewe kama mfugaji unapaswa kununua Kuku kwenye chanzo sahihi ili usijepata hasara.
Mnadani ni sehemu ambayo wafanyabiashara wanapeleka bidhaa zao Na kukuta Na wanunuzi wa bidhaa hizo. Pia kuna wafanyabiashara wa Kuku ambao Mara nyingi hukusanya Kuku kutoka vyanzo mbalimbali Na kuwaleta mnadani. Hivyo kwa mtu ambaye anataka Kuku wa kufuga mnadani sio sehemu sahihi ya kununua Kuku wa kufuga. Mana on ileile kwamba Kuku wa kufuga lazma ujue taarifa zake za nyuma kama vile kupewa chanjo Na vingine ili ujue unaanzia wapi Na pia kama katokea kwenye chanzo kizuri atakuwa hana shida yoyote, pia faida ya kununua kwenye chanzo kinachofahamika ni rahisi unapopata tatizo kurejea uliponunua nakupata ufumbuzi lakini Kuku wa mnadani ni vigumu kujua Kuku huyo katokea wapi hivyo unaweza kununua kumbe anaumwa Na baada ya kumfikisha nyumbani anakufa na itakuwa hasara.
Kwa ujumla sokoni na mnadani ni sehemu sahihi ya kupata Kuku wa kitoweo na sio wa kufuga.
Hitimisho, chanzo sahihi cha kupata Kuku wa kufuga ni kwa mfugaji ambaye anafuata taratibu zote za ufugaji kama kuwapa chanjo zote Kuku wake Na dawa ya minyio

Jumamosi, 18 Agosti 2018

Habari ndugu wadau wa kukukibiashara, tuwaombe ladhi kwa kutokuwa hewani kwa muda sasa, nikutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu pale tutakapo timiza taratibu za mtandao tutarudi hewani kama kawaida. Tunawaomba ladhi sana kwa usumbufu. Asante tunawatakia siku njema.

Jumamosi, 10 Februari 2018

Hii ni mifumo ambayo inatumika kufugia kuku Tanzania

Aina za ufugaji wa kuku
Kuna aina mbili za ufugaji wa kuku katika nchi ya Tanzania

1. UFUGAJI URIA

kuku wanajitafutia chakula wenyewe. Aina hii kuku hufungiwa bandani usiku lakini mchana hufunguliwa na kuachwa wajitafutia chakula na maji wenyewe kasha hurudi tena bandani usiku. Na ndio mfumo ambao kaya nyingi za kitamzania zinautumia.

Faida ya ufugaji uria

i. Hakuna gharama za chakula
ii. Kuku hujipatia aina mbali mbali za vyakula kama wadudu, majani na nafaka hivyo hujipatia mlo kamili.
iii. Mtaji, wake ni mdogo kwani hutumia ujenzi rahisi wa mabanda.
iv. Kuku wanaofungiwa kwa njia hii huwa na chanjo.
v. Kuku hawavunji mayai hawapigani, wala kunyonyoana manyoya.

Changamoto

i. Ni ngumu kuzuia minyoo na magonjwa.
ii. Kuku wadogo (vifaranga) huliwa na wanyama na ndege. Mayai hupotea na kuliwa na viumbe waharibifu.
iii. Kuku hupata shida ya mvua na baridi.
iv. Kuku wanaofungiwa kwa njia hii huwa na chanjo.
v. Nafasi kubwa huitajika kwa ajili ya kuwapa kuku nafasi ya kujitafutia chakula cha kutosha.

2. UFUGAJI NUSU URIA

Aina hii ya kuku hujengewa banda na uzungushiwa senyenge kuzuia kuku wasifike mbali na chakula na pia hujengewa sehemu ya kutaga mayai.

Faida

I. Ujenzi ni rahisi
ii. Mbolea usambaa kwa urahisi shambani
iii. Ni rahisi kuzuia na kukinga magonjwa.
iv. Ni rahisi kuokota mayai na pia mayai hayo hayaliwi na wanyama wasumbufu.
v. Hupungua gharama za chakula kwani kuku ujotafutia na kupewa kiasi kidogo cha nyongeza.

Kuna aina mbili za kufuga kuku wa ndani

i) battery cage system.
ii) deap litre system.

Tanzania hutumia njia deap litre system ambapo maranda ya mbao, majani ya mpunga, ngano na pumba za mchele hutumika sakafani kiasi cha 10-15 za ujazo.
- tandiko ambalo ubadilishwa mara tu linapobonyea au kuchanganyika na mbolea au kila baada ya miezi mitatu (3)
- kuku hupewa chakula, kuwekewa viota vya kutagia kuku afugwe kwa kufuata vipimo vya eneo ambavyo ni kuku 2-3 kwa 1m2
- banda hujengwa urefu wa 60 cm kwa tofali au udongo sehemu inayobaki huwa ni kwa kuruhusu mzunguko wa hewa.

Faida zake

1. Kuku wengi hufugwa katika sehemu ndogo
2. Kuku hupata kinga za hali ya hewa, mvua, jua na baridi. Pia hukingwa zaidi na wanyama wasumbufu kama mwewe, panya na nyoka.
3. Mayai hukusanywa kwa urahisi.
4. Kuku hufugwa kibiashara rahisi kukinga magonjwa na wadudu.
5. Mbolea hupatikana kwa wingi.

Changamoto

1. Chakula kisipochanganywa vizuri hakitumiki
2. Gharama kubwa hutumika kujengea banda.

Hizi ni aina za kuku wanaopatikana Tanzania

AINA ZA KUKU
kuna aina kuu mbili za kuku
1. Kuku wa asili ( kuku wa kienyeji)
2. Kuku wa kisasa

Kuku wa asili
Hawa utofautiana katika maumbo, utagaji, uzito, rangi ya manyoya, ukuaji na uwezo wa kutaga mayai. Kuku wa kienyeji hukua taratibu na utaga mayai machache.

Kuku wa kisasa (zaotic breed)
Hawa ni kuku toka nchi za kigeni pia wana aina mbili ambazo ni
i. Kuku chotara
ii. Pure breed

Kuku chotara
Ni mchanganyiko wa aina mbili au zaidi ya kuku. Siku hizi kuku wanaotakiwa kibiashara ni kuku chotara ( wengine ni wa mayai na wa nyama)

Pure breed
Hawa wanagawanyika sehemu mbili kuku (a) kuku wazito ( hutoa nyama) broiler
(b) kuku wepesi ( hutaga mayai) layers

Jumanne, 2 Januari 2018

Faida sita (6) za kutumia banda la kisasa (cage)

Karibu ndugu mfuatiliaji wa makala hizi za ufugaji wa kuku. Nimatumai yangu una afya njema ili kuweza kuwa pamoja na mimi katika kujifunza changamoto na namna ya kufanikiwa katika swala zima la ufugaji. Karibu leo katika mada nyingine inayohusu banda la kisasa ( kwa lugha ya kigeni inaitwa "cage") ambalo inafaida nyingi nzuri katika kupunguza changamoto mbalimbali za ufugaji wa kuku. Cage imeleta utofauti mkubwa japo ni gharama lakini ukitazama kwa jicho la tofauti au kwa kina utagundua ufugaji wa kawaida una changamoto nyingi ambazo zinaweza pelekea kufikia gharama za kuwa na cage.

Zifuatazo ni faida za kutumia cage (banda la kisasa)

1.kuzuia upotevu wa chakula. Banda hii limetengenezwa katika ubora ambao unawezesha kuku kupata nafasi ya kutoa kichwa nje ya banda na kula chakula chake bila kuchakua na mdomo au miguu ambayo mara nyingi ndio inayosababisha umwagaji wa chakula chini na kupelekea upotevu wa chakula kingi chini. Namna inavyokuwa ni kwamba kuku anakuwa kwa ndani lakini sehemu ya chakula ipo kwa nje.

2. Unatumia muda mchache kuhudumia kuku wengi. Hii ni faida nyingine ya banda hili la kisasa maana hapa tunaweza kuzungumzia ufugaji mkubwa wa kuku kuanzia kuku 200 na kuendelea. Namna ya kuwa hudumia wakiwa chini katika banda la kawaida ni changamoto, kwa namna ya kuwapa chakula, kuokota mayai kama ni kuku wa mayai, kusafisha banda n.k lakini matumizi ya cage hurahisisha namna zote kwa maana ulishaji wa chakula, kuokota mayai na kusafisha banda kwa urahisi ndani ya muda mfupi unaweza kuhudumia kuku zaidi ya 1000.

3. Hupunguza magonjwa ya kuambukizwa. Katika mabanda yetu ya kawaida kwa maana ya chumba ambacho kuku wanakuwa chini mara nyingi, kuku hula kinyesi chake au cha mwingine kulingana na eneo husika. Hivyo ni rahisi sana kwa kuku mgonjwa kuweza kuambukiza kuku wengine hasa kupitia kinyesi. Lakini hii ni tofauti ukitumia cage, kinyesi chote kinadondokea chini bila kufika katika sehemu nyingine ambapo kuku wapo.

4. Kujua idadi kamili. Kwa kawaida kuku wanaofugwa chini ni vigumu sana kuweza kuwa hssabu na kujua idadi kamili hasa kuanzia kuku mia na kuendelea na pia hata kama kuna wizi unafanyika kugundua si rahisi, lakini matumizi ya cage hurahisisha kuwa na takrimu sahihi za kuku wako, kwa sababu cage moja inakaa kuku 96 na ndani yake kuna visehemu ambavyo hukaa kuku wa 4 kila kisehemu. Hivyo ni rahisi kujua idadi ya kuku wako kila siku.

5. Inarahisisha zoezi la ukusanyaji wa mayai. Namna cage ilivyotengenezwa inaruhusu kuku kutaga na yai kushuka toka ndani na kuja nje ya banda ambapo kuna sehemu maalumu kwa ajili ya mayai yaliyotagwa ilikukusanywa kirahisi, tofauti na utaratibu wa kawaida tuliouzoea kuokota mayai chini. Ambapo muda mwingine kama kuku wana upungufu wa madini ya calcium hula mayai yake lakini kwenye banda hili hawezi fanikiwa kula yai kwa namna banda lilivyotengenezwa.

6. Inarahisisha kusafisha na kukusanya mbolea. Hili zoezi liko kama ifuatavyo, banda hili lina ngazi tatu kwa namna lilivyotengenezwa katika pande zote kushoto na kulia ila kila sehemu ya banda ambapo kuku hukaa ina uwazi wa kudondosha kinyesi chini bila kuangukia kwa wengine na kwa namna banda lilivyo kinyesi chote kitakuwa chini ambapo kuna uwazi mkubwa wa kuruhusu mfugaji kuweza kusafisha kwa urahisi na kuku sanya mboleo.

Himisho kwa faida za kuwa na zao bora la mradi wako. Tunashauriwa ni vyema tukatumia banda la kisasa. Lina matokeo mazuri zaidi, japo ni gharama lakini ubora wake ni maradufu ya ufugaji wa kawaida. Changamoto nyingi zinapungua katika matumizi ya cage ( banda la kisasa ). Napenda kuchukua fursa hii kukushukuru ndugu msomaji na mfuatiliaji kwa kuwa pamoja na mimi kuanzia mwanzo wa makala hadi kufikia hapa. Karibu tena katika mfululizo wa makala zijazo siku kama ya leo.

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

Jumatatu, 1 Januari 2018

Hizi ni faida za ufugaji wa kuku kama fursa

Fursa katika ufugaji wa kuku
Fursa ni changamoto au matatizo yaliyotuzunguka. Kwa maana nyingine ni vitu gani tunavipata kwa shida kati mazingira yetu ya kawaida katika pilika za kila siku na ndio mahitaji yetu. Hiyo ni fursa. Timekuwa tukipata shida jinsi ya kujua fursa zilizotuzunguka kutokana na kutojua neno fursa lina maana gani hasa kwa mapana yake. Tukija katika kona ya ufugaji wa kuku, fursa iliyopo ni changamoto tunazokumbana nazo kila siku katika ufugaji wa kuku aina zote. Tusilalamike tuu kuwa hatuwezi fanikiwa. Kayika mazingira yetu kuku kazoeleka kama utamaduni wa kila kaya ya kitanzania kuwa na kuku lakini anachukuliwa kama mfugo wa kawaida asiye na faida yoyote ile kuku ni fursa kubwa ambayo imeqatoa watu wengi kiuchumi. Tutumie nafasi tuliyonayo kujikwamua kiuchumi.
Hizi ni faida za ufugaji wa kuku kama fursa
Kuanza na mtaji mdogo. Hii ni moja kati ya faida za kuanzisha mradi wa kuku. Kqa kawaida mtu yoyote anaweza kuanzisha mradi huu wa kuku kwa sababu hauhitaji mtaji mkubwa ili kuanza. Mfano kuku mmoja ambaye ni mtetea ma jogoo mmoja unaweza kuanza kama mradi. Changanuo ufuatao unaonyesha ni kwa jinsi gani. Mtetea mmoja na jogoo unaweza kununua kwa elfu 25 kwa maana jogoo elfu 15 na mtetea 10, baada ya mwezi mtetea atakuwa ameanza kutaga na ndani ya mwezi. Kipindi amemaliza kutaga ukamuwekea mayai 10 na 15 ndani ya siku 21 atatotoa vyote au 10. Vifaranga 10 ukowa lea mpaka miezi 6 watakuwa kuku wakubwa na baadaya hapo wataanza kutaga na kulalia na kupata vifaranga wengi na ukaendelea kupata kuju wengi zaidI. Ndio maana unaweza kutumia mtaji mdogo na baada ya kuwa na kuku wengi na kuanza kuuza.
Chanzo chan mapato. Kuku ana bidhaa muhimu kama vile kuku, mayai,  nyama, na kinyeji. Vyote hivi ni mahitaji ya binadamu katika maisha ya kila siku. kupitia kufuga Kuku utapata fursa ya kutengeneza pesa nyingi tu. Kama utakuwa mfuatiliaji makini, kwa maana kuwapa chanjo kwa wakati, chakula bora na kutibu magonjwa pindi yakitokea. Kuku wa kienyeji aliyekoma anauzwa 15000, 20000, 25000, 30000 na kuendelea inategemeana na kuku mwenyewe. Tatizo kubwa tulilonalo Watanzania hasa kwa kuku wa kienyeji kadhalaulika na kuonekana ni wa kawaida lakini tukikaa kujua trei moja mayai ya kienyeji linauzwa 15000. Je? Ukiwa unaweza kuzalisha trai 5 kwa siku utakuwa na shilingi ngapi. Tuamke na kufanya ufugaji wa kuku kuwa wa uwakika.
Utawala wa mradi wa kuku ni rahisi. Urahisi huu hauna maana kuwa hakuna ugumu hapana ila maana kubwa ya hii pointi ni kwamba hatakama ni mfanyakazi wa kuajiliwa utapata muda wa kufuatilia kwa karibu maendeleo ya kuku wako. Mfano umeanza na mradi wako wa kuku 100 ,umewafugia nyumbani kwa kawaida unatakiwa kujipangia ratiba. Kwamba kabla ya kwenda kazi ni kufika bandani na kuwa hudumia kuku wako, hata kama utamwachia kijana aendelee kuwa hudumia kipindi ukiwa kazini, utakuwa unajua kuku wako wako salama. Pia jioni ukitoka kazini inabidi upate muda wa kipitia bandani na kuona hali ilivyo na kupata mrejesho kutoka kwa kijana uliyemwachia.
Soko la kuku ni kubwa Tanzania na nchi za nje pia.Hili swala ni fursa kubwa kwetu sisi vijana hasa ambao tumekuwa tukilalamikia ishu ya ajira za serikali na mashirika binafsi. Lakini tazama watu wa nje ya nchi na baadhi ya wenyeji wanaoingiza bidhaa za kuku kama, vifaranga, kuku na mayai. Wakati nafasi ya kuzalisha hapa hapa tunayo ni swala la maamuzi na kuacha kulalamikia serikali juu ya ajira. Vijana ajira tunayo mikononi mwetu ni swala la kuchukua hatua. Uwezekano upo kwa Tanzania kuanza kujihidumia yenyewe na kuanza kutoka nje ya mipaka pia. Takrimu zinaonyesha bado hata nusu ya matumizi ya kuku kwa ndani ya nchi, Cha msingi ni sisi kutafuta taarifa sahihi ili kuweza kufanya maamuzi sahihi. mojawapo ya chanzo kizuri cha taarifa za kilimo na ufugaji ni ESRF na youtube tazama knowledge tv.
Mradi wa kuku ni benki hai. Benki hai ni namna ya kuhifadhi pesa yako kwa matumizi ya baadae. Sasa ufugaji wa kuku ni benki hai maana yake ukiwekeza pesa yako katika kuku itakuwa sehemu salama na itaongezeka kwa kadri unavyozidi kuzalisha kuku wengi. Benki hii ni tofauti na benki za kawaida kwa sababu hakuna gharama yoyote ya makato ya uendeshaji, hapa ni kuhakikisha pesa yako inakuwa ni jitihada zako kuhakikisha unazalisha kuku wengi.
Nikutakie kila la heri kwenye kuazimisha mwaka mpya wa 2018 wenye mafanikio makubwa ya malengo yako na watu waliokuzunguka. Karibu sana katika ukurasa wetu facebook na kwenye whatsapp group ili uweze kujumuika na wafugaji wengine kubadilishana uzoefu na mafundisho mbalimbali kutoka kwa wataalamu waliobobea katika ufugaji wa kuki kisasa.

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

 

mail

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner