Wiki ya kwanza - 35°c
Wiki ya pili - 32°c
Wiki ya tatu - 29°c
Wiki ya nne - 26°c
KUROILER
Wafugaji wengi wa kuku wametamani sana kufuga mbegu bora ya kuku hasa wa kienyeji ili kupata matokeo mazuri katika biashara, hasa pale tunapozungumzia uuzaji wa kuku unategemea sana uzito wake, ambapo mbegu ya kuku wa kienyeji kwa mtetea ni uzito wa kilo 1.8 wastani na jogoo ni kilo 2.5, ambao ni uzito Mdogo sana labda kwa jogoo kidogo sio mbaya lakini kwa mtetea ni Mdogo sana kupeleka sokoni.Changamoto hii imepelekea wafugaji wengi kupoteza masoko na wengine kukosa kabisa. Hivyo basi kumepatikana sululisho la changamoto, maana kwa Tanzania sasa imepatikana mbegu bora kabisa inayokata kiu ya wafugaji wengi ambayo inaitwa KUROILER. Kuku huu ni mbegu chotara mwenye Sifa sawa na kuku wa kienyeji. Sifa zake ni kama zifuatazo
Wana rangi kundi
Kuku hawa wanavutia sana kwa kuwa tazama, kutoka na rangi zao nzuri. Wengi wake wanarangi ya kanga Yaani madoadoa. Pia sio hiyo tu wanarangi nyingine ambazo ukiwafuga wanavutia sana kuwatazama.
Chakula
Ulaji wa kuku huyu ni wa kawaida kama alivyo kuku wa kienyeji. Kwa maana ya kwamba anaweza jitafutia mwenyewe kwa kuachwa nne na kuokota wadudu mbalimbali pamoja na mabaki tofauti tofauti, pia kama utakuwa na utaratibu wa kununua chakula cha dukani anakula bila shida yoyote, kutengeneza mwenyewe kwa kununua mahitaji mbalimbali ambayo ni muhimu kwa chakula, mfano chakula vya protini, wanga, madini na chumivi. Vyovyote takavyo taka apate chakula chake anakula bila tabu. Bila kusahau pia unaweza mpa mabaki ya chakula nayo yanafaa.
Anafugwa kienyeji
Kuku huyu hutaga mayai lakini halalii, hivyo inambidi mfugaji achukue jukumu la kumlea kifaranga kama ambavyo mtetea angemlea. Hii inamaanisha kuwa kifaranga ataitaji joto cha chakula ili akue na baada ya miezi, utamwacha ajitafutie chakula mwenyewe kama ilivyo kwa kuku wa kienyeji. Anauwezo wa kutafuta chakula kwa kula wadudu, mabaki na vitu vingine ambayo vinafaa kuliwa
Utagaji wao
Kuku hawa wanauwezo wa kutaga kwa muda wa miaka 3 na hawalalii mayai yao.Mayai yao huwa na mbegu kwa maana ya kwamba, yai lenye mbegu maana yake kuku ametaga yai hilo kwa kupandwa na jogoo. Kumbuka kuku aina yoyote anauwezo wa kutaga yai bila kupandwa na jogoo na kutaga lakini yai hilo halitakuwa na mbegu ndani yake kama ilivyo kwa kuku wa kisasa wa mayai. Kwa maneno mengi yai yenye mbegu likilaliwa nitatoa kifaranga. Kingine yani la kuku huyu hufaa kuanguliwa. Pia idadi ya mayai ni 200 hadi 250 kwa mwaka.
Uzito wako
Kuku hawa wanauzito mkubwa ukilinganisha na kuku wa kawaida au kienyeji.Maana mtetea anaanzia kilo2 hadi 3 na jogoo anaanzia kilo 3 mpaka kilo5. Kwanza wanasifika kwa kuwa na nyama nyingi na watamu pia lakini sio kwamba kwa kilo hizi kuna maanisha hawa kui kwa muda sahihi lahasha kilo hizo ni kuanzia miezi mitano na kuendela.
Mayai yao
Mayai yao huwa na rangi huwa tofauti na kiini chake huwa cha njano.Na ili kupata kiini cha njano kama ilivyo kwa kuku wengine kuroiler anatakiwa ale majani. Kingine mayai yake ni makubwa kuliko ya kuku wa kienyeji na mara nyingi hutotolewa na machine ya kutotoleshea vifaranga.
Huhimili
Kuku huyu anahimili sana magonjwa kama ilivyo kwa kuku wa kienyeji. Cha muhimu ni kuzingatia chanjo kama zinavyoitajika, hii itakusaidia kuwakinga na magonjwa kama kideri na mengine
hitimisho
Baada ya kupata Sifa hizi za kuku aina ya kuroiler, chukua maamuzi sasa kwa kufuga mbegu bora na yenye faida kwa mfugaji tofauti na mbegu ya kienyeji kabisa ambayo haina mchanganyiko wowote. Ushauri nilikuwa na ufugaji mwenye faida ni kuwekeza nguvu, ajili na pesa katika Kuku ndipo utapata faida lakini vinginevyo tutaishia kuona fursa hii haina maslahi yoyote.
KABILA ZA KUKU WA KIENYEJI
Kuna makabila tofauti ya kuku wa kienyeji, ni ngumu kidogo kuweza kuyachanganua makabila hayo kutokana na muingiliano mkubwa wa vizazi kati ya aina mbalimbali za kuku hao. Hata hivyo kuku hawa wana tofauti za kimaumbile zinazosaidia kwa kiasi fulani kutambua uwepo wa baadhi ya makabila ya kuku. Kabila hizi pia zinahusishwa kwa kiasi kikubwa na eneo kuku wanakotoka. Baadhi ya kuku wa kienyeji wanaweza kutambuliwa kwa maumbile yao Mfano:
a. Kishingo - kuku wasio na manyoya shingoni
b. Njachama au Nungunungu - Hawa ni wale wenye manyoya yaliyosimama.
c. Kibwenzi - Ni wale wenye manyoya mengi kichwani.
d. Kibutu- Hawa hawana manyoya mkiani
Mwingiliano wa vizazi unaweza ukasababisha kuku kuwa na aina ya maumbile mchanganyiko. Mfano kuku aina ya kuchi anaweza kuwa na alama ya kishingo, Njachama, Kibwenzi au Kibutu.
Hivyo kabila za kuku zifuatazo zinaweza kutambuliwa kama ndiyo kabila za kuku wa kienyeji kulingana na maumbile yao na maeneo wanakotoka.
KUCHI
Ni kuku warefu kwa umbo na wenye kusimama mgongo ukiwa wima. Wana manyoya machache mwilinini na hasa kifuani, vilemba vyao ni vidogo. Majogoo huwa na wastani wa uzito wa Kg. 2.5 na mitetea kg 1.5 mayai ya kuchi yana uzito wa wastani wa gm 45. Kuku hawa hupatikana kwa wingi maeneo ya Mwanza, Shinyanga, Tabora na Zanzibar.
CHING'WEKWE
Kuku hawa ambao jina lao ni gumu kidogo kwa mtu asiyekuwa na meno kulitamka wana sifa zifuatazo.
Majogoo wana wastani wa kg 1.6, Mitetea wastani kg 1.2, mayai wastani wa gm 37. Kuku hawa wenye umbo dogo hupatikana zaidi maeneo ya CHAKWALE mkoani Morogoro na pia sehemu za umasaini. Kuku hawa hutaga mayai mengi sana kuliko aina nyingine ya kuku wa kienyeji waliopo Tanzania, kwa hiyo wanafaa sana kwa biashara ya mayai.
UMBO LA KATI
Majogoo wana uzito wa wastani wa kg. 1.9, Mitetea kg. 1.1, Kuku hawa ndio hasa wanaoitwa wa kienyeji(wa kawaida) Wana rangi tofauti. Utafiti umeonyesha kuwa kuku hawa hukua upesi na hupata kinga upesi baada ya kuwachanja dhidi ya ugonjwa wa mdondo (Castle desease)
Muhimu - Mfugaji akifanya uchaguzi kutoka kwenye aina hii ya kuku na kutoa matunzo mazuri kwa hao kuku waliochaguliwa, Hakika anaweza kupata kuku walio bora na wenye uzito wa kutosha pia kutaga mayai mengi na makubwa.
SINGAMAGAZI
Ni aina ya kuku wakubwa wa kienyeji wanaopatikana zaidi TABORA, kuku hawa wana utambulisho maalum kutokana na rangi zao. Majogoo huwa na rangi ya moto na mitetea huwa na rangi ya nyuki. Uzito - Majogoo uzito wa wastani wa kg 2.9, mitetea wastani wa kilo 2 mayai gramu 56.
MBEYA
Kuku hawa wanapatikana Ileje mkoani mbeya. Asili hasa ya kuku hawa ni kutoka nchi ya jirani ya Malawi na si wa kienyeji asilia bali wana damu ya kuku wa Kizungu "Black Australop". Majogoo Kg 3 mitetea kg 2 mayai gram 49
PEMBA
Hupatikana zaidi Pemba. Majogoo Kg.1.5 Mitetea Kg 1 mayai wastani gm 42
UNGUJA.
Majogoo Kg 1.6,mitetea kg 1.2 mayai gm 42. Kuku hawa wa Unguja na Pemba wanashabihiana sana na Kuchi isipokuwa hawa ni wadogo.
AINA ZA KUKU
kuna aina kuu mbili za kuku
1. Kuku wa asili ( kuku wa kienyeji)
2. Kuku wa kisasa
Kuku wa asili
Hawa utofautiana katika maumbo, utagaji, uzito, rangi ya manyoya, ukuaji na uwezo wa kutaga mayai. Kuku wa kienyeji hukua taratibu na utaga mayai machache.
Kuku wa kisasa (zaotic breed)
Hawa ni kuku toka nchi za kigeni pia wana aina mbili ambazo ni
i. Kuku chotara
ii. Pure breed
Kuku chotara
Ni mchanganyiko wa aina mbili au zaidi ya kuku. Siku hizi kuku wanaotakiwa kibiashara ni kuku chotara ( wengine ni wa mayai na wa nyama)
Muhimu
kuku wa kienyeji ni wazuri sana kwa kufuga kibiashara lakini matokeo mazuri ya kuku huyu ni pale atakapofugwa kisasa, hii inamaana kwamba inaitajika chakula kizuri chenye mchanganyiko uliokamilika, banda zuri lenye nafasi,chanjo mbalimbali muhimu kwa ukuaji,uangalizi wa karibu,kutunza kumbukumbu na kuchagua aina nzuri au kabila zuri la kufuga.